Mchungaji akiongoza ibada ya Kuaga Mwili wa Marehemu Willy Edward leo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri nchini,Absalom Kibanda akisoma historia fupi ya
Marehemu Willy Edward wakati wa Kuaga mwili wake leo kwenye Viwanja Vya
Mnazi Mmoja jijini Dar.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe akizungumza kwenye shughuli hiyo ya kuaga Mwili wa Marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba akitoa neno kwa
wafiwa wakari wa shughuli ya Kuaga mwili wa Marehe Willy Edward leo.
Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi akimpa pole Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Jambo Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo
Leo,Juma Pinto wakati wa Shughuli ya Kuaga mwili wa Marehemu Willy
Edward ambaye alikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Jambo leo,iliyofanyika leo
kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar.
Baadhi
ya Wahariri wa Vyombo mbali mbali vya Habari hapa nchini wakijiandaa
kushusha jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo,Marehemu
Willy Edward Ogunde aliefariki dunia mwishoni mwa wiki mkoani
Morogoro.Shughuli ya kuaga Mwili wa Marehemu Willy imefanyika leo katika
viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar na baadae ikafuatia safari ya kwenda
Nyumbani kwao Mara kwa Mazishi.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe akitoa heshima zake.
Bw. Athuma Hamis akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima zake
za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa Mhariri wa
Gazeti la Jambo Leo aliefariki ghafla huko mkoani Morogoro mwishoni mwa
wiki.Hafla hii ya kuaga imefanyika mchana huu katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,Jijini Dar.
Mwili wa Willy Edward ukiwekwa katika sehemu yake tayari ibada ya kuaga.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini,Absalom Kibanda akibadirishana mawazo na Mkuu wa Masoko wa Benki ya NMB,Iman Kajura.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo Mbali mbali vya habari nchini wakiwa katika picha ya pamoja.
Ankal akiwa na Mwanalibeneke Francis Godwin
Ankal
akisabahiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim
Lipumba,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnaupe pamoja na
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginald Mengi.
Mwili ukipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya Mara kwa Mazishi.
Waombolezaji.Picha Zote Kwa Hisani ya Michuzi Blog
Comments