
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amemfuta kazi mkuu wa polisi Generali Bheki Cele, aliyekuwa ametuhumiwa kwa makosa ya rushwa.
Bwana
Zuma aliambia waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake na pia kuhusu
atakayechukua nafasi yake akiwa ni bwana Mangwashi Phiyega.
Hatua hii inamfanya bi Mangwashi kuwa mkuu wa kwanza wa polisi mwanamke.
Generali
Cele, ambaye mtangulizi wake alifungwa jela kwa tuhuma za ufisadi,
alihukumiwa mwezi Oktoba baada ya taarifa kuhusu kuhusika kwake katika
kashfa uuzaji haramu wa nyumba za polisi ingawa alikanusha madai hayo.
Inaaminika alihusika na kampeini ya rais Zuma wakati wa kampeini za uchaguzi wa rais mwaka 2009.
Mwaka
jana afisa anayechunguza kesi za ufisadi ,Thuli Mandonsela, alisema
kuwa nyumba za polisi zilikodiwa kutoka kwa kampuni moja ambayo
ilipandisha bei ya kukodi na kwamba Cele ndiye alihusika na kashfa ya
kupandisha bei ya nyumba hizo.
Bi Madonsela ambaye ni mratibu wa malalamiko ya umma alimshtumu Generali Cele kuwa mmoja wa wale waliohusika na kashfa hiyo.
Alichunguza
utaratibu wa kukodisha nyumba ambazo zilikuwa za polisi mjini Pretoria
na mji wa Mashariki wa Durban na kupata kweli zilipandishwa bei kinyume
na sheria. Serikali ya Afrika Kusini imekumbwa na kashfa nyingi za
ufisadi katika siku za hivi karibuni. Chanzo :http://www.bbc.co.uk/swahil
Comments