Wana DMV wakisikiliza kwa makini maelezo ya ukopeshaji mikopo ya nyumba.
- Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu pamoja na mkurugenzi mkuu wa TMRC (Tanzania Mortgage Refinance Company) na Mkurugenzi Mkuu Azania Bank, pamoja na Maofisa wa benk mbali mbali.walipokuwa na Jumuia ya waTanzania waishio DMV siku ya Ijumaa June 1, 2012 kwenye ukumbi wa Mirage Hall, wakizungumzia utaratibu mzima wa suala la mikopo ya nyumba (Tanzania Mortgage Refinance Company)
- Katika mkutano huo wa uwekezaji, Tanzania Mortgage Refinance Co.Ltd(TMRC), walipata fursa ya kuwaeleza utaratibu mzima wa maisha ni nyumba, pamoja na kujijibu maswali mbali mbali yalioulizwa na wana Jumuia ya Watanzania waishio hapa na kuelimisha zaidi katika mkutano huo ili nae Mtanzania aliekuwepo njee ya nchi kufaidika zaidi kwa mradi huo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) .Inatoka kwa mdau .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments