WANAWA
K E wanaotumia dawa au kuchoma sindano k u o n g e z a makalio na
viungo vingine vya mwili wametahadharishwa kuwa wanaweza kupata ugonjwa
wa saratani.
Aidha, wanawake wanaotumia mashine kutaka kusimamisha matiti wametahadharishwa huenda wakashindwa kunyonyesha watoto baadaye wakati wanaotumia vifaa maalumu kuridhisha hamu zao za kimapenzi wameelezwa kuwa wataathirika kisaikolojia.
Daktari Ali Mzige akizungumza na HabariLeo Jumapili katika mahojiano maalumu yaliyozaa habari hii, alisema anashangazwa na wanawake na mabinti wa Kitanzania wanaohangaika
kunywa dawa na kuchoma sindano kwa lengo la kuongeza makalio au sehemu zingine za viungo vya miili yao huku wakihatarisha afya zao, ikiwa ni pamoja na kupata saratani bila kujua.
Mzige alisema wako wanawake wengine wanatumia vifaa maalumu ili kujiridhisha kimapenzi na kwamba wanaotumia vifaa hivyo huathirika kisaikolojia bila kufahamu na ndio hao baadaye wanakataa hata kuolewa kwa sababu tayari wameathirika.
“Wanawake hawafahamu wanaiga tu, huko Ulaya wanaofanya mambo haya ya ajabu ni waathirika wa dawa za kulevya au tayari unakuta wameathirika kisaikolojia, lakini sisi tunataka kuiga tu k la kitu badala ya kutumia vitu vya asili,” alisema.
Dk. Mzige ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya IMTU, alisema haoni makalio makubwa
yanawapa faida gani wanawake na kwamba uvutaji wa matiti una husisha uvutaji wa misuli inayoshikilia nyama za matiti na matokeo yake baadaye mhusika anakuja kushindwa kunyonyesha mtoto.

Comments