|
Naibu
Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya kuingia
ofisini humo kuanza kazi, kutokana na afya yake kuimarika. Mwakyembe
amekuwa akitibiwa nchini India kwa muda mrefu. Picha na Zacharia Osanga |
BAADA ya utata wa muda mrefu wa ama Naibu Waziri wa
Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amelishwa sumu au la, jana Mbunge huyo wa
Kyela, aliweka hadharani ugonjwa wake akisema unafahamika kitaalamu
kwa jina la Popular Scleroderma huku akisisitiza: “Sasa nimepona
kabisa.”Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo
mwaka jana yalizidi kumtikisa na Oktoba 9, Serikali iliamua kumpeleka
Hospitali ya Appolo, India kwa ajili ya matibabu na uchunguzi
zaidi.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam
jana, Dk Mwakyembe akiwa amevalia kofia ya pama alisema: “Si kwamba
sijambo, bali nimepona kabisa baada ya kugundulika na maradhi hayo na
kutibiwa.”“Nimerudi juzi kutoka India na daktari wangu ameniambia
nimepona, nilikuwa nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Scleroderma’
iliyosababisha ‘skin disorder’ (ngozi kutokuwa katika hali ya kawaida),
lakini kwa nguvu za Mungu nimepona, namshukuru Mungu.”
Kuhusu sumu
Alipoulizwa kuhusu tuhuma za kulishwa sumu, Dk Mwakyembe alikataa
kuzungumzia hilo akisema anasubiri uchunguzi ulioagizwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.Hata hivyo, Dk Mwakyembe
alisema angependa kuona uchunguzi huo unakamilika haraka na ripoti yake
inatangazwa kwa umma.Alisema yuko tayari na anasubiri tume hiyo ya
uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nahodha imhoji ili atoa kile kilichomo
katika ripoti ya daktari wake.Dk Mwakyembe alisema anachoshukuru hadi
sasa ni kwamba afya yake imeimarika kutokana na shinikizo la Rais
Jakaya Kikwete ambaye aliagiza Serikali kumpa kipaumbele wakati wote
akiwa nchini na India hatua ambayo imemwezesha kufika hapo
alipo.Kutokana na hali hiyo, Dk Mwakyembe aliwataka wananchi wote
wakiwemo wa jimboni kwake Kyela kuondoa wasiwasi akisema sasa yupo
imara kwa ajili ya ujenzi wa majukumu ya taifa.“Ninaomba wapiga kura
wangu wa Kyela waache jazba, wawe na subira juu ya matatizo yangu. Wiki
ijayo nitakwenda kuzungumza nao ili niweze kuwaeleza matatizo
yaliyokuwa yananisumbua, lakini sasa hivi niko fit,” alisema.
SOMA ZAIDI
:http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/21277-dk-mwakyembe-aweka-hadharani-ugonjwa-wake
Comments