Picha ya pamoja uongozi wa TUGHE Taifa na Uongozi wa TCIA
Mandhar ya ukumbi wa mkutano
washiriki wa mkutano wakifuatilia kwa makini
Meza kuu wakiimba wimbo wa Mshikamano
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
Uwazi, na ushirikishawaji hupunguza migogoro kazini.
IMEELEZWA
kuwa uendeshaji wa taasisi kwa uwazi , usikivu wa viongozi na uongozi
wa pamoja kati ya menejimenti na wafanyakazi katika kupanga mipango na
kuweka maamuzi mbalimbali ndio nguzo kuu ya uboreshaji wa mahusiano
mahali pa kazi.
Hayo
yalisemwa leo (jana) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga
Tanzania(TCAA) ,Fadhili Manongi wakati akizungumza na mwandishi wa
habari hizi mara baada ya kutia saini mkataba mpya wa Ushirikishaji wa
Wafanyakazi na Baraza la Wafanyakazi na Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya(TUGHE) na mamlaka hiyo.
Utiaji
saini wa mkataba huo wa miaka mitatu ulifanyika katika ofisi za makao
makuu ya mamlaka hiyo ambapo viongozi mbalimbali wa pande zote hizo
walisaini. Miongoni mwa viongozi waliotia saini makataba huo ni
Manongi, Katibu Mkuu Msaidizi Taifa(TUGHE), John Sanjo na Katibu wa
TUGHE Mkoa wa Dares Salaam, Gaudensi Kadyanga.
“Hakuna
matatizo katika tawi letu pale inapotoekea tofauti tunakaa chini
tunaelezana.hivyo ni vizuri kwa viongozi mahali pa kazi kuwa wasikivu
wa mambo mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi kwa kuwa wao ndio wanaojua
mambo mengi kuliko sisi tunavyojua.
“Hivyo
kuna umuhimu wa kuwashirikisha wafanyakazi mambo mbalimbali na bajeti
kwa kuwa wanaweza kuishauri menejimenti ili kuweza kupunguza athari
zitakazoweza kujitokeza,” alisema Manongi.
Aliongeza
kuwa pia yanapotoea mafanikio mahali pa kazi ni vizuri kutoa maotisha
kwa wafanyakazi ili kupunguza migogoro na uchangia kuongeza ari ya
kufanya kazi.
Naye
Mwenyekiti wa Tawi la TUGHE la mamlaka hiyo, ambaye pia alitia saini
mkataba huo, Eugene Lwala alisema mamlaka hiyo imefanikiwa kuboresha
mahusiano hayo kutokana kuwa viongozi wa pande hizo zote mbili
kuheshimu mipaka yao ya kazi , kuvumiliana na vikao vya mara kwa mara.
Comments