Nchi
yetu itasitisha rasmi matumizi ya teknolojia ya utangazaji ya analojia
na kuhamia teknolojia ya dijitali ifikapo tarehe 31 Desemba, 2012 saa
sita usiku.
Lengo la kufanya hivyo ni
kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano duniani
kote,Miongoni mwa faida za kutumia teknolojia ya dijitali ni kuongezeka
kwa ubora wa matangazo ya televisheni, ongezeko la chaneli za
televisheni litakalotokana na matumizi bora ya masafa, kuwepo kwa masafa
ya ziada yatakayopatikana baada ya kuzimwa kwa mitambo ya analojia
inayotumia masafa mengi, kuongezeka kwa watoa huduma wa mawasiliano ya
simu, matangazo ya televisheni kupatikana katika vifaa vingi zaidi vya
mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa
intaneti.
Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano inakua kwa kasi sana na hivyo kuwa kichocheo
katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Kufuatia kasi ya ukuaji wa
teknolojia, sekta ya utangazaji ipo katika mabadiliko kutoka mfumo wa
teknolojia ya analojia kwenda mfumo wa wa digitali duniani kote. Hii
inatokana na changamoto zinazoikabili teknolojia ya analojia ikiwemo
uhafifu wa picha na sauti, matumizi makubwa ya masafa na nishati, pamoja
na teknolojia inayopitwa na wakati ya kurushia matangazo ya aina hiyo.Ndi
Comments