.Nathan
Mpangala Kwa wiki kadhaa sasa yuko mafunzoni nchini Mexico, akihudhuria
kozi fupi ya waandishi wa habari, inayohusu Civil Resistance and Non
violence Conflict. Hapa akiwa na baadhi ya washiriki wenzake toka
sehemu mbalimbali duniani, wakiandaa michoro kwa ajili ya video
itakayotumika kwenye kampeni ya familia zilizopoteza ndugu, jamaa na
marafiki kutokana na mauaji ya kila siku yanayohusishwa na biashara ya
dawa za kulevya.
Nathan
Mpangala pia usiku huu ameshinda tuzo ya wachoraji bora wa katuni
katika tuzo za (AJET) zilizoandaliwa na Baraza la Habari (MCT)
zinazofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
salaam.
Hapa wakiendelea na kazi yao ya kuandaa katuzi hizo zinazohusu mauaji yanayotokana na madawa ya kulevya nchini Mexico.
Comments