Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (kulia)
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya
kuchezesha droo ya kwanza ya mwezi kupitia promosheni ya M-pesa ili
kupata mshindi wa shilingi Milioni kumi, wa pili kulia ni Afisa Masoko
wa M-pesa Reenu Verma, na Meneja wa Mifumo ya kompyuta Bw. Patrick
Makungu pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania
bi. Chiku Saleh.
Mwakilishi
wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Chiku Saleh (kushoto)
akinukuu namba ya simu ya mshindi wa shilingi milioni kumi aliepatikana
katika droo ya kwanza ya mwezi iliyochezeshwa na Kampuni ya simu za
mkononi Vodacom Tanzania kupitia promosheni ya M-pesa, wa pili kushoto
ni Meneja wa Mifumo ya kompyuta wa kampuni hiyo Bw. Patrick Makungu
katikati ni Afisa Masoko wa M-pesa bi. Reenu Verma, anayeshuhudia
(kulia) ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa Vodacom Rukia Mtingwa.Inatoka kwa mdau fullshangwe.
Comments