Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowasa
(katikati) akizungumza na Meneja Mahusiano wa Benki ya NMB,Shy-Rose
Bhanji ambaye amefika Wilayani Monduli jana kwa kutoa msaada wa sh. 10
milioni uliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya wahanga wa Mafuriko
yaliyoukumba mji wa Mto wa Mbu,Wilayani Monduli.Kulia ni Meneja wa Benki
ya NMB Kanda ya Kaskazini,Vicky Bishubo.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Mh. Jowika Kasunga (kulia) pamoja na DAS wa
Monduli,George Mjema wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.Inatoka kwa mdau Mjengwa.
Comments