[Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa]
LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA, NEC YAVIONYA CCM, CHADEMA
Na Waandishi Wetu
KANISA
Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa
Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za
ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.Akizungumza kwa
simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus
Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo
halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.
Akizungumza
katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira
alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa
ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi
ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.
Hata
hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu
Ruwaichi alijibu kwa kifupi: “Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye
vyombo vya habari, hii leo siyo habari.”
Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.
“Kanisa
halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama
Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli
ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake,” alisema
Ruwaichi.
Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.
“Ukiona
mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika,
vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa,”
alisema.
Askofu
Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za
kuchafuana... “Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia
mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za
kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na
hatuna vipaumbele.”
Askofu
Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala
yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo
yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi
kuchagua viongozi bora.
Kauli
hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa
kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo
Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.
“Kama
tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia
mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu,”
alisema Dk Slaa.Soma zaidi www.mwananchi.co.tz
Comments