MKATABA
wa Benki ya NMB na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umefikia tamati
tangu Desemba mwaka jana, na taarifa za ndani zinadai kuwa taasisi hiyo
kubwa ya fedha nchini haina tena mpango wa kuingia mkataba mpya.
NMB iliingia mkataba wa udhamini na TFF kwa muda wa miaka mitano wenye thamani ya Sh400milioni kila mwaka.
NMB iliingia mkataba wa udhamini na TFF kwa muda wa miaka mitano wenye thamani ya Sh400milioni kila mwaka.
Msemaji
wa TFF, Boniface Wambura alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba ni
kweli mkataba wao na benki hiyo umekwisha tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Kuhusu
taarifa kwamba benki hiyo haina tena nia ya kuingia mkataba mpya,
Wambura alisema taarifa zilizopo ni kwamba wako kwenye mazungumzo ya
kuingia mkataba mpya.
"Ni kweli
mkataba na NMB umekwisha tangu mwaka jana mwishoni, kwa sasa tumefungua
milango ya mazungumzo ili kuangalia makubaliano mapya," alisema
Wambura.
Kauli ya Wambura ilikuwa sawa na ile ya Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Imani Kajula.
Akiongea na Mwananchi jana, Kajula alisema mkataba na TFF umefikia tamati, lakini hata hivyo bado kuna fursa na mazungumzo zaidi kuangalia uwezekano wa kudhamini tena.
Akiongea na Mwananchi jana, Kajula alisema mkataba na TFF umefikia tamati, lakini hata hivyo bado kuna fursa na mazungumzo zaidi kuangalia uwezekano wa kudhamini tena.
NMB ilikuwa ikiidhamini TFF kila mwaka kwa miaka mitano mfululizo na imekuwa ikitoa Sh400milioni kila mwaka.
Katika udhamini huo NMB walikuwa wakisaidia maeneo matatu, Taifa Stars ambayo ilikuwa ikipata Sh150milioni, Timu ya Taifa ya Vijana (Serengeti Boys) Sh150milioni na TFF Sh100milioni ambazo zilitumika kwa ajili ya shughuli za kiofisi.

Kufuatia
hali hiyo, mkutano mkuu wa TFF wa kawaida wa mwaka uliokuwa ufanyike
mwaka jana kwa mujibu wa katiba, ulishindikana na badala yake umepangwa
kufanyika mwishoni mwa Aprili.
Katika
mkutano huo ambao habari zilizopo ni kuwa unadhamini na kampuni ya
Said Salim Bakharesa, pamoja na mambo mengine utajadili pia suala la
Kampuni ya Klabu za Ligi Kuu, uanachama wa mikoa mipya, ambayo ni
Katavi, Njombe, Geita, Simiu ikiwa ni pamoja na suala zima la mapato
na matumizi ya shirikisho pamoja na Uchaguzi Mkuu, utakaofanyika
mwishoni mwa mwaka huu.
Source:Mwananchi
Comments