Rais Jakaya Kikwete akizungumza katika moja ya mikutano hivi karibuni
Na Tiganya Vincent-Arusha
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
anatarajia kufungua mkutano wa Kimataifa wa Mamlaka za Kuzuia na
Kupambana na Rushwa kutoka nchini mbalimbali .
Kauli hiyo imetolewa leo(jana) na Msemaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Doreen Kapwani wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizo mjini Arusha.
Kapwani
amesema kuwa hii ni mara ya kwanza mkutano wa namna hiyo kufanyika
nchini ambapo zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia
kushiriki mkutano huo wa siku tatu.
Amesema
kuwa mkutano huo unatarajia kushirikisha Nchi kama vile Morocco ,
Uingereza, Qatar, Uganda, Romania, Brazil, Austria, india, Belgium ,
Spain, Ukraine , Malsiyia , Namibia na Mwenyeji Tanzania.
Kwapwani amesema kuwa mkutano unafanyika hapa nchini wakati Tanzania imepata heshimiwa kubwa ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri juu ya Rushwa ya Umoja wa Afrika Machi mwaka huu.
Comments