KIZAZI kijacho huenda kisijue nini hasa maana ya Bagamoyo, mji uliokuwa na
barabara ya kwanza ya uhakika, mji wa kwanza makao makuu ya koloni la Kijerumani
na bandari ya kwanza kusafirisha pembe za ndovu na watu kama bidhaa.
Kwa wale wanaopenda kuujua mji wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani, wataujua kwa namna ambavyo wao wanapenda kuujua. Lakini, kwa wanazuoni na watafiti wa masuala ya jamii na historia yao, ni dhahiri mji huu unatoweka katika mazingira yao kwa spidi ya mwanga, ingawa wenyeji hawalioni hilo.
Nilipata bahati ya kwenda Bagamoyo hivi karibuni. Nilifikishwa na waungwana pale kwenye Msalaba, lakini niliporudi katika nyumba niliyofikia, niliwafikiria wote wanauzuru Bagamoyo.
Naam, wanaozuru Bagamoyo wawe wale wa kidini, kihistoria au kwa burudani, kitu kimoja kiwazi kabisa Bagamoyo mji wenye fursa na changamoto za kimaendeleo, unakuwa mji wa kisasa, ukizima historia iliyopo polepole, na mimi nathubutu kusema unakufa kihistoria,
wakazi wake hawana cha kujivunia.

Comments