MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA OFISI ZA TAWI LA CCM MWANAKWEREKWE B, MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka
Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa
Mjini Magharibi, Unguja jana. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo,
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta
jambo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mjini Magharib, Mohammed Yussuf, wakati
alipofika mkoa huo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za
Tawi la CCM Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto) na mmoja kati ya wazee wa
eneo hilo ambaye ni kati ya wazee waliokuwa na kucheza ‘Chandim’ pamoja. Hapa
ilikuwa ni baada ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Ofisi za Tawi la CCM
Mwanakwerekwe B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja jana.
Comments