Mwanamitindo
wa kimataifa wa Tanzania, Millen happiness Magese akipiga picha ya
pamoja na washindi watatu waliopata tiketi ya kuonyesha mavazi katika
wiki ya mitindo ya Afrika Kusini, Victor Casmir, Victoria Casmir na
Anastazia Gura katika picha ya pamoja. wengine katika picha ni Aminat
Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12 (wa kwanza
kushoto), Ritha Poulsen (wa kwanza kulia) na Mustapha Hassanali
aliyesimama nyuma.
***
Wanamitindo
watatu, Anastazia Gura (21) na mapacha, Victoria Casmir (20) na Victor
Casmir wameshinda usaili uliondeshwa na kampuni ya Millen Magese Group
Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani
ya mitindo ujulikanao kwa jina la Tanzania International Fashion Exposé
(TIFEX).
Wanamitindo
hao wamefanikiwa kupita katika usaili huo ambao uliwajumuisha
wanamitindo 350 kutoka katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es
Salaam na mikoa ya jirani.
Kutokana
na ushindi huo, wanamitindo hao wanatarajia kuondoka mwishoni mwa mwezi
huu kuelekea nchini Afrika Kusini kushiriki kwa mara ya kwanza katika
historia katika fani ya mitindo ya wiki ya mitindo ya Afrika Kusini
maarufu kwa jina la South Africa Fashion Week.
Akizungumza
baada ya usaili huo, Millen alisema kuwa amestushwa sana na ujio wa
wanamitindo mbali mbali mbali waliofika katika usaili huo japo
alitangaza kwa muda mfupi.
Millen
alisema kuwa awali alipanga kuchukua wanamitindo wawili, lakini
kutokana na idadi kubwa iliyojitokeza, ameongeza nafasi moja kama
shukrani yake ya witikio huo mkubwa.
Alisema kuwa walipata kazi kubwa sana kuchagua wanamitindo hao watatu, lakini kwa kushirikiana na wanamitindo maarufu Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12 na Ritha Poulsen, waliweza kufanikisha zoezi hilo mapema zaidi.
Millen alisema kuwa washindi hao wamepata fursa pekee ya kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.
Alisema
kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na
vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya
mitindo na hata kwa njia ya utalii.
Aliongeza
kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo
kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika
Kusini na Nigeria.
Comments