Jumuiya
ya Afrika Magharibi ECOWAS imesimamisha uanachama wa Mali kuafuatia
hatua ya jeshi kuoindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure .
Viongozi wa Jumuiya hiyo walifikia uamuzi huo katika mkutano uliofanyika nchini Ivory Coast.
Sasa viongozi hao kutoka nchi sita wanachama wa ECOWAS wamepanga kusafiri hadi mjini Bamako Mali ili kukutana na baraza kuu la jeshi linalotawala nchi hiyo.
Akihutubia waandishi wa habari baada ya mkutano huo Rais wa Ivory Coast, alisema Amadou Toumani Toure bado yuko hai na yuko katika hali njema .
Kiongozi huyu wa Ivory aliongezea kuwa alizungumza na Toure saa chache kabla ya mkutano wao kuanza.
Na kwa wale waliohusika na kumwangusha madarakani rais wa Mali, ECOWAS imechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kusitisha uanachama wao katika chombo hiki, kulaani mapinduzi hayo ya kijeshi na kutishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo iwapo viongozi wapya wa kijeshi hawatarejesha utawala wa katiba.
Nae mwenyekiti mpya wa Tume ya ECOWAS, Kadre Desire Ouedraogo, ametoa wito wa kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa na kumchagua Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso kuwa msuluhishi wao.

Comments