LWIZA KUSIMAMIA EL MERREIKH, PLATINUM CL
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Kisongole Lwiza kuwa Kamishna wa mechi ya Ligi ya Mabingwa (CL) kati ya El Merreikh ya Sudan na FC Platinum ya Zimbabwe.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza itachezwa Aprili 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa El Merreikh jijini Khartoum, Sudan kuanzia saa 2 kamili usiku. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wikiendi hii jijini Harare timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
El
Merreikh ni moja ya timu ambazo CAF iliziingiza moja kwa moja katika
raundi ya kwanza. FC Platinum iliingia raundi ya kwanza baada ya
kuing’oa Green Mamba ya Swaziland katika raundi ya awali.
ZIMBABWE YAITAKA TWIGA STARS
Chama
cha Mpira wa Miguu Zimbabwe (ZIFA) kimeomba mechi ya kirafiki kati ya
timu yake ya Taifa ya wanawake na Twiga Stars. Mechi hiyo itakayochezwa
kati ya Aprili 28 au 29 mwaka huu jijini Harare.
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya timu ya Zimbabwe kwa ajili ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Twiga Stars ambayo iko
kambini mkoani Pwani tangu Machi 25 mwaka huu chini ya Kocha Charles
Boniface Mkwasa nayo inajiwinda kwa fainali hizo ambapo itacheza mechi
ya kwanza Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa dhidi ya Ethiopia. Zimbabwe yenyewe inacheza na Senegal.
Machi
10 mwaka huu, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenella Mukangara alizindua akaunti ya Twiga Stars kupitia Tigo Pesa kuichangia timu hiyo ili ishiriki vyema michuano ya AWC.
Wachangiaji wa Twiga Stars wanatakiwa kutuma mchango wao kwenda namba
13389 ambapo kiwango cha juu kinachoweza kutumwa kwa muhamala
(transaction) mmoja ni sh. 500,000. Katika uzinduzi huo, Waziri Dk.
Mukangara alichangia sh. milioni moja.
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI
Mtihani kwa ajili ya mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Machi 31 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Watu
watatu wamejitokeza kufanya mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.
SIMBA, YANGA ZASAKA POINTI VPL
Yanga na Simba ni miongoni mwa timu nne zitakazokuwa viwanjani kesho (Machi 31 mwaka huu) kusaka pointi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambayo iko katika raundi ya 22.
Uwanja
wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi namba 148 kati ya
Coastal Union na Yanga. Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Rashid
Msangi wa Dodoma ambaye atasaidiwa na Rashid Lwena (Ruvuma) na Issa
Malimali (Ruvuma).
Mwamuzi
Amon Paul wa Musoma ndiye atakayechezesha mechi namba 151 kati ya
African Lyon na Simba itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Viingilio
kwenye mechi ya African Lyon na Simba ni sh. 3,000 kwa viti vya kijani
na bluu, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B
wakati VIP A ni sh. 15,000.
Aprili
Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi ya VPL kati ya Azam na Ruvu JKT
itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Kiingilio katika mechi
hiyo kitakuwa sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 jukwaa kuu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments