| Kalunde Jamal UHABA wa vifaa vya kitabibu nusura ugharimu maisha ya kipa Moro United, Dickson Chove aliyegongwa na mshambuliaji Nsa Job wa Villa Squad na kuzimia kwa dakika kadhaa kwenye Uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam, juzi Jumatano.Kuzimia kwa Chove kumekuja ikiwa ni wiki chache tangu dunia iliposhudia kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba akinusurika kifo kutokana kukwama kwa mishipa ya moyo iliyosabisha kuzimia uwanjani. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu uliozikutanisha timu za Moro United dhidi ya Villa Squad kwenye Uwanja wa Azam Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwepo kwa gari la wagonjwa wala vifaa sahihi vya kitabibu kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji wanapoumia uwanjani hapo. Chove aligongana na Job alipokuwa akijaribu kumzuia asifunge na kupoteza fahamu ndipo viongozi na madaktari walipoingia uwanjani kwa lengo la kumsaidia wakiwa mikono mitupu. Daktari na viongozi hao walipofika haraka waliamua kumvua jezi na kuanza kumpepea bila ya mafanikio na kuamua kumtoa nje na kumwingiza kwenye vyumba uwanjani hapo huku wakiwa wamembeba kichwa chini miguu juu. Kama hiyo haitoshi uwanjani hapo hakukuwa na gari la wagonjwa la kumuwahisha hospitali mchezaji huyo au mitungi ya gesi ya kumsaidia kupumua. Soma zaidi: http://www.mwananchi.co.tz/michezo/16-kandanda/21573-chove-yamkuta-ya-muamba |
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments