Mwenyekiti wa CHADEMA Mkuranga, Jamal Lwei
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkuranga amesema leo asubuhi akitoa
salamu za pole kwa baadhi ya wanamkuranga waliofikwa na maafa kutokana
na mvua zilizoambatana na upepo siku ya jana , ambapo taarifa za awali
zinabainishwa kuezuliwa kwa mapaa ya baadhi ya nyumba za wananchi wa
wilaya hiyo na nyingine kuangukiw na miti.
Mwenyekiti huyo pamoja na mambo mengine pia amezungumzia uchaguzi wa
Arumeru Mashariki huku akisisitiza kuwa ana imani wana Arumeru
watamchagua Nassari kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusimamia sera za
kimaendeleo.
Duru za kisiasa kutoka jimbo la Mkuranga ambalo linashikiliwa na Adam
Malima zinabainisha kuwa watu wengi wanahamia CHADEMA Kutokana na sababu mbalimbali
pamoja na kushindwa kwa sera za CCM za maisha bora kwa kila mtanzania
huku wananchi wakiendelea kusota kwenye umasikini mkubwa huku viongozi
wa serikali hasa wale wateule wa rais Kikwete wakiogelea kwenye
utajiri mkubwa. Baadhi ya wananchi wameenda mbali zaidi huku wakihoji
kuhusu mgao wa umeme, matokeo mabovu ya shule za sekondari na msingi
pamoja na huku wakiishinikiza serikali iwalipe malipo ya fedha za
korosho ambazo wamesema bado hawajalipwa.
Na Novatus Kambota
Comments