Wananchi
mbalimbali wakiwa wamebeba Jeneza la aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la
Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo katika Msikiti kwa ajili ya
Kumsalia.Marehemu alifariki hapo jana katika Hospitali ya Mnazi
Mmoja Mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein
wakatikati akijitayarisha pamoja na viongozi mbalimbali kwa ajili ya
Kumsalia marehemu Salum Amour Mtondoo,kulia kwake ni Makamo wa kwanza
wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi na kushoto
yake anaejitengeneza kanzu yake ni Mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar
Kabi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Sheikh Ali Mohd Shein
wakatikati akiwa pamoja na waislamu wengine katika dua ya kumuombea
aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo
katika msikiti wa Bububu.Kulia kwake ni Makamo wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi na kushoto yake ni Mufti Mkuu wa
Zanzibar Sheikh Omar Kabi na wambele alieshika maiki ni Msomji wa Dua
hio Sheikh Halfan.
Waheshimiwa
mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria katika kumuambea Dua
aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo
hapo katika Msikiti Mkuu wa Bububu Mjini Zanzibar.
Mufti
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabi mwenye Maik akiomba Dua kwa ajili ya
kumuambea aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour
Mtondoo hapo katika Msikiti Mkuu wa Bububu Mjini Zanzibar.kulia kwake
ni Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein na mwengine ni Makamo wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi.na kushoto ya sheikh ni
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi na mwengine ni
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho.
Katibu
wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhili Soraga akitoa Mawaidha katika
mazishi ya aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Zanzibar Marehemu
Salum Amour Mtondoo huko Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein
akiongoza wanananchi mbalimbali katika mazishi ya aliekuwa Mwakilishi
wa Jimbo la Bububu Zanzibar.Mazishi hayo yaliofanyika huko kijijini
kwao Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Spikawa
Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akitoa hotuba ya Shukrani kwa
Viongozi na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Mazishi ya
aliyekua Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo
aliezikwa huko kijijini kwao Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.16/03/2012.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.16/03/2012.
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 16/03/2012
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed
Shein leo ameongoza mamia ya wananchi wa Zanzibar katika mazishi ya
aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu (CCM) Salum Amour Mtondoo
yaliyofanyika katika kijiji cha Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika Mazishi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiwamo Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim
Seif Shariff Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Spika wa
Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan
Mwinyi yalitanguliwa na sala iliyofanyika katika Msikiti wa Bumbwini Misufini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed
kwa niaba ya Serikali ilitoa hisia zake za kuguswa na msiba huo na kuwaomba
wananchi wa Jimbo la Bububu na wanafamilia kwa ujumla kuwa wastahamilivu
katika kipindi hiki kigumu.
Aidha Waziri Aboud amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na
wanafamilia katika kipindi hiki sambamba na kutoa ubani kwa ajili ya wanafamilia
hao ikiwa ni njia ya kuwafariji.
Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema kifo cha Mwakilishi
huyo ni pigo kwa wananchi wa Zanzibar,Jimbo la Bububu na Baraza la
Wawakilishi kutokana na utendaji kazi alioukuwa nao.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameri Kificho kwa upande wake ametoa
shukrani kwa Viongozi na wananchi ambao walishirikiana nao tokea kipindi cha
kuumwa marehemu hadi kifo chake.
Spika Kificho amesema marehemu Mtondoo alikuwa ni mtu mtulivu na mwenye
mashirikiano makubwa kwa wenziwe na kuwataka wananchi wa Jimbo la
Bububu kumuomba Mungu ili wapate kiongozi bora kama marehemu.
Marehemu Salum Mtondoo ambaye amefariki dunia jana katika Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Bububu ,
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar
uliofanyika Octoba, 2010.
Marehemu Mtondoo alizaliwa tarehe 14/ 12/ 1962 huko Bububu, Wilaya ya
Magharibi , Zanzibar ambapo alipata elimu yake ya msingi na Sekondari katika
Skuli ya Bububu kuanzia mwaka 1969 hadi mwaka 1979.
Aidha katika katika shughuli za kisiasa, Marehemu amewahi kushika nyadhifa
mbali mbali katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo Mjumbe wa Kamati ya
siasa ya Tawi na nafasi za ujumbe katika jumuiya ya wazazi Wilaya hadi Mkoa.
Marehemu Mtondoo nje ya siasa katika uhai wake aliwahi kufanya kazi ya
Usimamizi wa Kiwanda cha COTEX mnano mwaka 1983 hadi mwaka 1985 na
Baadae kufanyakazi za Ujenzi katika ushirika wa BBB 1986 hadi mwaka 1992.
Mbali ya kazi hizo, Marehemu aliwahi kufanyakazi za biashara kuazia mwaka
1992 hadi mwaka 2010.
Marehemu ambaye amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shindikizo la damu
ameacha wake watatu (Vizuka) na watoto 10.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dk.Jakaya
Kikwete kufuatia msiba huo ametuma salamu za rambi rambi kupitia Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai pamoja na viongozi mbali mbali wa
Bara na Visiwani.
Huyu ni Mwakilishi wa pili kufariki dunia kupitia Chama cha Mapinduzi ambapo
Mwakilishi wa kwanza kufariki alikuwa Marehemu Mussa Khamis Silima wa
Jimbo la Uzini kwa ajali ya gari ambaye pia alikuwa Mbunge wa kuchaguliwa
kupitia Baraza la Wawakilishi
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin.
Imetolewa na Maelezo Zanzibar 16/03/2012
Comments