Mshutuko wa moyo |
Watu wengi wanafahamu kuwa matatizo ya moyo hasaa mshtuko wa moyo yanaweza tu kuwapata watu wazee.
Lakini kuna takriban vifo miatano huripotiwa kila mwaka nchini Uingereza kutokana na watu walio chini ya umri wa miaka 30.
Wakati
ikitokea ni picha ya kushtua. Hasa hasa inapotokea kwa nyota wa
michezo kama Fabrice Muamba mwenye umri wa miaka 23 pekee.
Fabrice ni mmoja wa wachezji walio na afya nzuri zaidi katika kilabu chake, Bolton Wanderers.
Matamshi sawa na hayo yalitolewa kuhusu marehemu Marc-Vivien Foe, aliyekuwa mchezji wa Cameroon.
Marc-Vivien alianguka na kupoteza fahamu, wakati wa mechi ya kimataifa mwaka 2003.
Lakini kinachosababisha vifo kama hivi huwa sana kutokana na mtu kurithi ugonjwa fulani kuliko hali ya kiafya ya mtu.
Hitilafu
katika celi za mwili ndio chanzo kikubwa cha mipigo isiyo sawa ya moyo
au ugonjwa wa misuli ya moyo ujulikanao kama "Cardiomyopathies".
Inawezekana
hali ya mtu inaweza kumfanya kupata mshutuko wa moyo, licha ya kuwa
anafanya mazoezi kila siku na wala hasongwi sana na mawazo. Hii ni kwa
mujibu wa Daktari mmoja mtaalamu wa matibabu ya moyo Leonard Shapiro.
Sasa ikawaje mtu mwenye kufanya mazoezi moyo
wake kusimama? Hili kwa kweli halijulikani vyema. Lakini utafiti
unapendekeza kuwa wale waliorithi matatizo ya moyo uwezekano wa moyo wao
kusimama ni mara mbili sawa na wale wanaoshiriki michezo inayohitaji
nguvu nyingi.
Daktari
Leonard Shapiro, ambaye ni mtaalamu wa matibabu ya moyo pamoja na kuwa
mshauri wa shirikisho la soka Uingereza, FA, anasema ni vigumu
kufahamu chanzo cha mshtuko wa moyo.
Lakini
anasisitiza kuwa kuna mambo kadhaa yanayoweza kumfanya mtu kupata
mshutuko wa licha ya kuwa anajihusiha sana na mazoezi yanayohitaji
nguvu nyingi.
Sasa je , nini kinaweza kufanyika ili kuzuia matukio kama haya?
Vitengo
mbali mbali vya michezo nchini Uingereza hufanyia wachezaji ucgunguzi
wa kiafya, ingawa sio lazima, kama ilivyo katika baadhi ya nchi , mfano
Italy.
Sio kamili
Katika
soka, wachezaji hufanyiwa uchungiz wa kiafya wakiwa na umri wa miaka
16 na kisha kupata ukaguzi zaidi katika siku za baadaye.
Wengi wanaopatikana kuwa na matatizo yoyote, huwa hawaruhusiwi kushirki kwenye michezo ya hali ya juu.
Daktari wa moyo katika michezo, Sanjay Sharma, anasema kuwa ukaguzi huo ni wa kiwango cha juu lakini sio kamili.
Ukaguzi
wenyewe unahusu kuchukua historia ya kiafya ya mchezaji kuhusu maradhi
ya moyo, kufahamu ikiwa mchezaji huhisi uchungu kifuani wakati
akipumua na hata kuuliza maswali kuhusu historia ya familia kwa sababu
matatizo mengi ya moyo hutokana na kurithi.
Hata
hivyo ukaguzi huu sio hakikisho kuwa mchezaji hawezi kuwa matatizo ya
moyo baadaye na tatizo kubwa zaidi huwa matatizo hayo huwa sio ya
kudumu.
Hujitokeza
tu na kisha kutibika, sawa na hali ya Muamba. Imesemekana kuwa Muamba
amefanyiwa ukaguzi wa moyo mara nne tangu aanze kucheza soka, wa hivi
karibuni ukifanywa mwaka jana
Chanzo:BBCInatoka kwa mdau Mjengwa.
Comments