WADAI ALIUZA NCHI AKIWA IKULU, CCM WAHAHA KUVUNJA MAKUNDI, NASSARI AAHIDI KUREJESHA ARDHI ILIYOPORWA
Waandishi
Wetu, Arumeru, JOTO la kuwania ubunge katika Jimbo la Arumeru
Mashariki, mkoani Arusha linazidi kupanda. Jana Chadema kilimgeukia
Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye aliongoza uzinduzi wa kampeni za
CCM juzi kikidai kwamba kiongozi huyo hana uadilifu wa kushiriki
kampeni za uchaguzi huo mdogo.
Madai hayo ya Chadema kwa Mkapa yalitolewa katika mikutano iliyofanyika katika Kata za Legaruki, Poli, Selunani na Sing’isi, siku moja baada ya Mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM kusema chama hicho cha upinzani hakina sera zinazoweza kuwakomboa wana Arumeru na kuwataka wasimchague mgombea wake, Joshua Nassari.
Kadhalika, Mkapa katika mkutano huo ulifanyika kwenye Uwanja wa Ngaresero, Usa River, alimshambulia Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere akisema katika kuishi na kufanya kazi na Hayati Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kusikia jina la Vicent likitajwa katika ukoo huo wa Baba wa Taifa.
Jana, mbunge huyo ambaye ni Meneja Mwenza wa kampeni za Chadema katika uchaguzi huo alimjia juu Mkapa akisema kiongozi huyo si mwadilifu akidai kwamba ndiye chanzo cha matatizo mengi yanayolikabili taifa kwa sasa.
“Tuliwahi kusema kuhusu Mzee Mkapa na tukapata wito kwamba tumwache apumzike baada ya kustaafu lakini inavyoonekana hapendi kupumzika na badala yake amekuja hapa (Arumeru) na kuanza kutuchokonoa.
Mimi nasema huyu mzee siyo mwadilifu kwani alifanya madudu mengi alipokuwa Ikulu,” alisema Nyerere na kuongeza::
“Eti jana (juzi) aliwaahidi kwamba atashughulikia matatizo ya ardhi, kwani aliyesababisha matatizo haya yote ni nani?…. ni yeye. Halafu yeye sasa siyo Rais, siyo diwani wala mbunge, kwa hiyo hana uwezo wowote wa kutatua matatizo yenu, wala msidanganyike.”
Nyerere alidai kwamba utawala wa Mkapa ni mbaya kuliko mwingine uliowahi kutokea nchini kwani ulisababisha mauaji Kisiwani Pemba kiasi cha Watanzania wengine kugeuka wakimbizi baada ya kukimbilia eneo la Shimoni, Mombasa, Kenya.
Mbunge huyo wa Musoma Mjini alisema matatizo ya ajira nchini ni matokeo ya ubinafsishwaji wa viwanda vyote uliofanywa na Serikali ya Mkapa... “leo hii ukiwa mijini huwezi kujua nani ni kichaa na nani mzima, vijana wengi wanaokota makopo. Ni bingwa wa kuuza kila kitu, aliuza benki zote na aliuza viwanda vyote na sasa hivi tunavyozungumza viwanda vingi vimegeuzwa magodauni (maghala) ya kuhifadhia bidhaa za Wachina badala ya kuwa vitovu vya ajira kwa vijana wetu.”
Nyerere alidai pia kwamba Mkapa ni kiongozi pekee ambaye baada ya kukaa madarakani miaka 10, kisha kupata fursa ya kulipwa pensheni ambazo ataendelea kuzipata maisha yake yote, aliingiwa na tamaa ya mali, hivyo kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira.
“Kama tusingetumia nguvu ya umma kuudai mgodi huo asingeurudisha, sasa mtu wa aina hiyo ana kitu gani cha kutuambia hapa Arumeru?... Kama kweli ana uadilifu, basi aje hapa kesho atujibu ili tumwambie madudu yake mengine aliyofanya akiwa Rais,” alidai Nyerere.
Kuhusu uhusiano wake na Baba wa Taifa, Nyerere alisema kimsingi yeye ni mwanafamilia kwani Baba yake, Mzee Kiboko Nyerere alikuwa ndugu wa damu wa Julius Nyerere na kwamba Mkapa si mwanafamilia hiyo hivyo hawezi kufahamu masuala ya familia yao.
Soma zaidi:http://www.mwananchi.co.tz

Comments