Maafisa
wa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC wakiwa na Mwanamuziki Maarufu wa
nyimbo za injili nchini Tanzania Flora Mbasha na mumewe. Kutoka kushoto,
Emmanuel Mbasha, Ms. Maganga, Flora Mbasha, Mindi kasiga na Alex
Kassuwi
Mwimbaji
maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania, Flora Mbasha atembelea
Ubalozi wa Tanzania katikati ya jiji la Washington DC, Marekani.
Mtumishi huyu wa Mungu kupitia muziki wa injili alipata nafasi kuwa
mgeni wa Mh. balozi Mwanaidi Sinare Maajar siku hiyo, ambapo Mhe, balozi
huyo alizungumzia fursa mbalimbali zipatikanazo nchini Marekani na
Tanzania. Aidha Flora Mbasha alimmwagia sifa Mhe, balozi kwa mafanikio
makubwa ya kuwaunganisha watanzania walioko huku ughaibuni. Pamoja na
hayo Flora Mbasha alimshukuru Mheshimiwa balozi kwa kazi yake nzuri hapa
nchini Marekani. Zaidi ya hayo Flora alitoa shukrani za kipekee kwa
watanzania waishio nchini Marekanina kwa ukarimu wao, upendo na
mshikamano miongoni mwao.Mwisho Flora alitoa shukrani za kipekee kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya M. Kikwete kwa
kuweza kuendeleza amani na mshikamano nchini Tanzania.
Comments