Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika mkutano wa hadhara kata ya Msambweni Tanga.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionesha tunzo
maalum aliyokabidhiwa na Wazee wa Tanga kutoka na mchango wake kwa
amani ya Zanzibar.Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu Wa Kwanza Wa
Rais Zanzibar
-----
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amewataka
wanachama na wapenzi wa Chama hicho katika Mkoa wa Tanga kuacha
kuyumbishwa kwa mambo yasiyokuwa na msingi, na badala yake waungane
katika kikiimarisha Chama hicho.
Amesema
Chama hicho kiko imara na kitaendelea kuimarika kutokana na uwezo wa
viongozi wake ambao wamepata sifa kubwa duniani kutokana na umahiri wao
wa masuala ya uchumi na siasa.
Maalim
Seif ametoa changamoto hiyo katika eneo la Msambweni Tanga wakati
akiwahutubia maelfu ya wanachana na wapenzi wa Chama hicho
waliojitokeza kwa ajili ya kumsikiliza na kujua mwelekeo wa Chama hicho
baada ya kupata misukosuko ya kuwatimua baadhi ya viongozi wake.
Amesema
Chama hicho siku zote kimekuwa mstari wa mbele katika kusimamia misingi
ya haki na usawa kwa wananchi wote, na kwamba hakitosita kufanya hivyo
kwa kuangalia maslahi ya mtu binafsi.
Maalim
Seif amewapongeza wananchi wa Tanga kwa kumpa mapokezi makubwa wakati
akipowasili katika uwanja wa ndege wa Tanga, hali inayodhirisha uhai wa
chama hicho katika mkoa huo na maeneo mbali mbali Tanzania bara na
Visiwani.
Amesema
mapokezi yake ambayo yanathibitisha kuwa Tanga ni ngome ya CUF ambayo
haiwezi kubomoka, na yale ya Prof. Lipumba yaliyofanyika Dar es Salaam
tarehe 11/03/2012 yatakuwa dira ya kukiimarisha zaidi chama hicho na
kasi hiyo itaendelezwa hadi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Maalim
Seif amekebehi kwa wale wanaodai kuwa CUF ni CCM ‘B’ kwamba “wana wivu
wa kisiasa”, na wanaumwa na maendeleo ya chama hicho, na kuweka wazi
kuwa CCM na CUF havijaungana na wala havitoungana ikizingatiwa kuwa
kila chama kina sera zake.
Akiwasilisha
salamu za mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba
kwa wakaazi wa Mkoa wa Tanga amewataka kusimama imara na kujipanga
katika kutoa maoni ya katiba mpya, ili kuhakikisha kuwa katiba inaweka
wazi suala la maliasili kuwa rasilimali za Watanzania.
Amesema
Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi zikiwemo dhahabu, almasi,
Tanzanite, copper na madini mengine kadhaa, lakini bado rasilimali hizo
hazijawanufaisha wananchi kutokana na kutokuwepo utaratibu unaoeleweka
juu ya mgawano wa rasilimali hizo.
Amesema
Watanzania wanaweza kunufaika moja kwa moja na mgawano wa rasilimali
hizo, hali ambayo itapunguza utegemezi wa chakula, mfumko wa bei na
kupunguza umaskini kwa wananchi.
Katika
salamu hizo Maalim Seif amesema Tanzania inahitaji uongozi wenye dira
ya kuikomboa Tanzania kiuchumi, kwa kuweka mipango imara ya kiuchumi
ikiwa ni pamoja na kuimarisha miundombinu na kuvutia wawekezaji wa
sekta mbali mbali, jambo ambalo limekosekana kwa kipindi kirefu.
Katika
mkutano huo Maalim Seif alikabidhiwa tunzo maalum kutoka kwa wazee wa
Tanga kutokana na ujasiri wake wa kurejesha Amani Zanzibar.
Mkutano
huo ulikwenda sambamba na kumtambulisha na kumnadi mgombea wa udiwani
wa chama hicho kata ya msambweni Bw. Abrahman Hassan Omar, ambapo
amewataka wanachama kumchagua mgombea huyo ili aweze kusaidia
kuwatatulia kero zao.
Nae
Mgombea udiwani wa CUF kata ya Msambweni Bw. Abrahman Hassan Omar
amesema haombi uongozi ili apate kuwa bwana mkubwa bali kuwatumikia
wananchi wakati wote.
Naibu
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chama hicho bw. Sheweji Mketo
amewatahadharisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya
tarehe 01/04/2012, huku akiwataka wananchi wasishawishike kwa chochote
na waelewe kuwa siku hiyo itakuwa “April fool”.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
Comments