Khadija Khamis-Maelezo Zanzibar 12/03/2012
Makamu
wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad amesema changamoto
zinazotokea katika utendaji kazi katika Taasisi mbali mbali ni chachu
katika kuleta maendeleo na kujikwamua pale tulipofika.
Amesema
bila ya kuwa na changamoto maendeleo yataendelea kusuasua kwani
kutakuwa hakuna hatua itakayopigwa mbele katika kuleta mafanikio.
Maalim
Seif aliyaeleza hayo leo wakati akizungumza na uongozi wa Vyombo vya
Habari vya Serikali ikiwemo Idara ya Habari Maelezo,Shirika la
Utangazaji Zanzibar ZBC na Gazeti la Zanzibar ikiwa ni mfululizo wa
kutembelea Idara za Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo.
Amesema
vyombo vya habari ndio kiungo kikubwa kati ya wananchi na Serikali
hivyo ni vyema kufanya kazi kwa uadilifu na kuweza kukabiliana na
vikwazo ambavyo vinaweza kurudisha nyuma juhudi mbali mbali
zinazochukuliwa na wananchi na hata Serikali.
Akizungumzia
juu ya mafunzo kwa wanahabari, Maalim Seif alizitaka taasisi hizo kuwa
na mpango mzuri wa kuwapeleka waandishi wa habari masomoni na katika
mafunzo mengine ili waweze kukabiliana na kasi ya maendeleo ya
teknolojia ambayo kwa sasa inakwenda kwa kasi kubwa.
Amesema
masomo humjengea uwezo mwana habari wa kuweza kutumia kifaa chochote na
kuweza kuibua mambo kadha ikiwemo uwezo wa kumkabili mtu yeyote bila ya
woga au wasi wasi.
Amewataka
waandishi wa habari katika Idara hiyo kuendelea kuwa wabunifu katika
uandishi na kuandika habari zilizofanyiwa utafiti wa kina bila ya woga
wowote
Maalim
Seif alisisitiza haja ya kuwa na vifaa vya kisasa vinavyokwenda na
wakati ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi , haraka na kwa wepesi zaidi.
Mapema
Makamu wa Kwanza wa Rais aliipongeza Idara ya Habari kwa utendaji wake
hasa kwa vile inatoa huduma ndani na nje ya nchi na kuishauri kuanza
kupeleka taarifa zake katika vituo vyengine vya kigeni kama BBC,AFP CNN
na REUTERS ili kuweza kutumia taarifa hizo na kuitangaza Zanzibar.
Akizungumzia
suala la mishahara alisema kuwa viwango vya mshahara kwa wafanyakazi wa
Vyombo vya habari ni vidogo kulingana na hali halisi na kupendekeza
viwango hivyo kubadilishwa kulingana na wakati uliopo.
“Binadamu ni binadamu anaangalia maslahi yake tukisema uzalendo tu wengi watashindwa”alisema Maalim Seif
Katika
Ziara hiyo Maalim Seif alitembelea Idara ya Habari Maelezo,Shirika la
Magazeti ya Serikali,Shirika la Utangazaji la Zanzibar ZBC pamoja na
maeneo ya Mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika hilo.
Comments