Muungano
wa Afrika AU umeelezea wasiwasi kutokana na mapigano ya mpakani kati ya
Sudan na Sudan ya Kusini, huku kukiwa na taarifa za mashambulio ya
angani yakiendelea.
Hali ya kutoelewana kutokana na mafuta ndio kizuizi kikubwa zaidi kati ya mataifa ya Sudan na Sudan ya Kusini kufikia muwafaka.
Muungano wa Afrika, AU, umeelezea wasiwasi mkubwa kutokana na mapigano yaliyozuka kati ya Sudan na Sudan ya Kusini.
Kufuatia siku mbili za mapigano, mkuu wa AU, Jean Ping, ameyashauri mataifa hayo mawili kuheshimu hatua ya kuwaondoa wanajeshi wao hatua ya kilomita 10 kutoka mpakani.
Ripoti ambazo bado hazijathibitishwa zinaeleza kwamba mapigano yamesitishwa, lakini Sudan iliendelea na mashambulio ya angani katika eneo la Sudan ya Kusini wakati wa usiku.
Mataifa hayo yalipambana vikali na kwa muda mrefu katika, katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, kabla hatimaye Sudan ya Kusini kufanikiwa kujitenga na kuwa taifa huru.

Comments