Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga,
akizungumza na wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tuzo za waandishi wa
habari (EJAT) itakayofanyika hivi karibuni, pamoja na waandishi wa
habari wakati akishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kufuatia
msaada wa shilingi milioni 10.925.000 ilioutoa kwa baraza hilo kwa
ajili ya maandalizi ya tuzo hizo, katika mkutano uliofanyika kwenye
makao makuu ya baraza hilo Mwenge jijini Dar es salaam, katika picha
katikati ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia
ya Serengeti (SBL) na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri
Absalom Kibanda.
Teddy
Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
akifafanua jambo katika mkutano huo kuhusiana na udhamini wao katika
tuzo hizo, kulia ni Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Absalom Kibanda,
ambalo limesaidia sana MCT kupata udhamini huo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akikabidhi mfano wa hundi yenye
thamani ya shilingi 10.925.000 kwa Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji wa
Baraza la Habari (MCT) , fedha ambazo Kampuni ya (SBL) imetoa kwa
Baraza la Habari (MCT) kwa ajili ya kufanikisha tuzo hizo, katikati ni
Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti.
Kutoka
kulia ni Imani Lwinga Meneja wa Habari na mawasiliano kampuni ya bia ya
Serengeti, Absalom Kibanda Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Teddy
Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano (SBL), Kajubi Mukajanga Katibu
Mtendaji (MCT) na Nandi Mwiyombela Meneja wa Mahusiano ya Umma wa
(SBL), wakionyesha mfano wa hundi hiyo kwa wajumbe wa kamati ya
maandalizi na waandishi wa habari.
Comments