“ Kifaransa- Lugha ya Umoja”
Nchi
13 zenye uwakilishi wa kidplomasia hapa Tanzania, zimeandaa kwa pamoja
tamasha la utamaduni na michezo kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya
utamaduni wa Kifaransa tarehe 20 Machi hadi 31 Machi, 2012.
Nchi
56 ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kifaransa(
International Organisation of Francophonie –OIF) na 19 zenye uwakilishi
wa utazamaji ambazo zinaongea Kifaransa duniani, zitasherehekea wiki
hii kwa lengo la kukuza lugha ya Kifaransa chini ya msingi wa mshikamo
wa lugha na tamaduni mbalimbali za kimataifa
Nchi
wanachama wa OIF zenye ofisi za kibalozi Tanzania, ni Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) ,Msumbiji, Ubelgiji, Vietnam; Kanada, Misri;
Uswisi, Ufaransa, Burundi, Rwanda, Jibuti, Shelisheli na Komoro kwa
pamoja zimeandaa tamasha la utamaduni na michezo kuadhimisha wiki ya
utamaduni wa Kifaransa katika miji ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar,
kama ifuatavyo:
Tarehe
20 Machi 2012- Ufunguzi wa maadhilisho utafanyika Forodhani- Kwenye
Hoteli ya Slipway iliyoko Masaki Dar es Salaam. Ufunguzi rasmi
atafanywa na Balozi wa DRC nchini, Mr. Juma Alfani Mapango na baadae
bendi yenye asili ya Kongo; Junior Ringo Kalunde & Band
itatumbuiza. Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni; Utalii
na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Abdillahi Jihad
Hassan
Tarehe
23 Machi 2012 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mheshimiwa Marcel
Escure, atamkaribisha Raisi wa Uchaguzi wa Kameruni Daktari Samuel
Fonkam Azu kutoa mada juu ya malengo ya OIF katika kudumisha demokrasia,
haki za kibinadamu na utawala wa sheria ili kuzua migogoro, namna ya
kujinasua kutoka kwenye matatizo; mpito kuelekea demokrasia na kudumisha
amani. Warsha hiyo itafanyika kwenye Asasi ya Kifaransa ya Dar es
Salaam “ Alliance Française de Dar es Salaam”
.
Tarahe
24 Machi 2012, Mwanamuziki mwenye kipaji na muimbaji kutoka nchi ya
Ivori, Dobet Gnahore atacheza albamu yake mpya katika Ukumbu wa
Utamaduni wa Kijerumani “ Goethe Institut” iliyopo Upanga; Atakuwa na
kikundi chake cha wachezaji.
Asasi ya Kifaransa ya Dar es Salaam ( Alliance Française) imealika kikundi cha sanaa cha kuigiza cha Kifaransa “Cie Pied la Route”
kuigiza tamthilia ya Mtunzi wa Kitabu cha hadithi kutoka Ivori,
Ahmadou Kourouma “ Mungu hakulazimika” ( Allah n’est pas oblige).
Kinahusu tamthilia ya wapiganaji- watoto na viongozi wa kivita katika
nchi za Liberia na Sierra Leone katika miaka ya 90. Mchezo utachezwa kwa
lugha ya Kifaransa na maandishi ya maelezo kwa iingereza.
Mashindano
ya ujuzi wa lugha ya Kifaransa yameandaliwa nchini kote kuanzia Mwezi
Februari ambapo wanafunzi 1, 700 watashiriki. Sherehe ya kutoa tuzo kwa
washindi wa mashindano hayo zitafanyika Allience Française tarehe 31
Machi 2012.
Juhudi
za kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Kifaransa zilianzishwa na
wakuu watatu wa Nchi za Kiafrika mwaka 1970; ambao ni Leopold Senghor
wa Senegali, Habib Bourguiba wa Tunisia, Hamad Dioro wa Niger na Mtoto
wa Mfalme Sihanouk wa Kambodia. Nchi 21 wilikubaliana kutia saini
mkataba wa kuanzisha ACCT ambapo mwaka 1988 Jumuiya ikabadilishwa
kuitwa OIF. OIF ni Jumuiya ya jamiii inayounganishwa na lugha ya
Kifaransa- katika Kifaransa “ Ceux qui ont le Français en partage”.
Jumuiya hii ina malengo ya kisiasa, kitamaduni na kiuchumi. Dira ya
jumuiya hii iko katika malengo manne ambayo yamekubaliwa na wanachama
wake:
Kukuza lugha ya Kifaransa na uwiano wa Kitamaduni na lugha
Kukuza amani, demokrasia na haki za binadamu
Kusaidia sekta ya elimu, mafunzo, elimu ya juu na utafitii
Maendeleo endelevu na mshikamano
Hivi sasa lugha ya Kifaransa, ni lugha ya kwanza au ya pili kwa zaidi
ya watu millioni 200 duniani, nusu yao wakiwa wanaishi katika bara la
Afrika na ni lugha rasmi ya mashirika mengi ya Kimataifa na yale ya
Kikanda likiwamo Umoja wa Afrika
Katika
Tanzania kumekuwa na ongezeko la watu wanaojifunza Kifaransa katika
ngazi mbalimbali zikiwemo za kitaalamu. Muamko huu ni jambo la kutia
moyo kwa kuwa nchi hii inazungukwa na baadhi ya nchi jirani zinazoongea
Kifaransa na ambazo zinajipanga kukuza utalii na zimeonyesha ari kubwa
ya kujiunga na Jumuiya za Kiuchumi na Kisiasa za Kanda ya Afrika.
Tujikumbushe kuwa nchi wanachama mbili ambazo ziko katika Jumuiya ya
OIF Rwanda na Burundi zilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Julai 1,
2007 .
Matokeo
ya muamko huu ni kuanzishwa kwa programu ya miaka 3 ya kuwafunza
waalimu wa Kifaransa ambayo imebuniwa na Serikali ya Ufaransa, Wizara ya
Elimu na Mafunzo Ustadi, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania ambayo inaendelea kutekelezwa.
Maadhimisho
ya Kifaransa duniani, ni sherehe za kimataifa za kuendeleza tamaduni
mbalimbali kupitia Kifaransa. Lugha ya Kifaransa ni daraja ambalo watu
na nchi zenye tamaduni mbalimbali hupita kuelezea asili zao. Ni jukwaa
la maelewano ambalo linaimarika kwa mahusiano na lugha na tamaduni
nyingine kama: Kiingereza, Kiarabu, Kireno na Kihispaniola. Kifaransa ni
lugha ya Kimataifa ambayo idadi ya wasemaji wake inakua kila kukicha.
Na jukwaa hili lenye tamaduni mbalimbali zenye lengo la kuuunganisha
dunia linaitwa : Ufungamano wa Tamaduni.
Comments