
BARAZA la madiwani la halmashauri ya mji Mpanda katika mkoa wa Katavi limepitisha mapendekezo ya bajeti ya hamashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 kwa ajili ya shughuli za maendeleo
Mwandishi
wa mtandao huu kutoka Mpanda mkoani Katavi Willy Sumia anaripoti kuwa
baraza hilo lilioketi leo Machi 9, 2012 limekubali kuyapitisha
makadirio na makisio ya bajeti ya halmashauri hiyo ambapo mweka hazina
wa Halmashauri hiyo Tatu Kisori amesema katika kipindi cha 2012/13
halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 606,847,000 kutoka
katika vyanzo vya ndani ambapo pia halmashauri yake inatarajia kupokea
ruzuku toka serikali kuu kiasi cha shilingi 6,441,517,240.
Amesema
katika ruzuku ya serikali kiasi cha shilingi 5,338,014,240/= ni malipo
ya mishahara kwa watumishi wa kada mbali mbali na shilingi
1,103,503,000/= ni za matumizi ya kawaida na kufafanua kuwa katika
bajeti hiyo mishahara ni ongezeko la asilimia 20 kutoka shilingi
4,265,057,000/= hadi 5,338,014,240/=
Akizungumzia
miradi ya maendeleo mweka hazina huyo alisema katika bajeti ya
maendeleo halmashauri yake inatarajia kutumia shilingi 3,870,010,627/=
kutoka serikali kuu, katika fedha hizo miradi ya maji imepewa
kipaumbele kikubwa kwa kutengewa asilimia 34 ambayo ni shilingi
1,300,288,600/= ikifuatiwa na idara ya utawala kwa asilimia 26 sawa na
shilingi 1,027,733,000/= pamoja na elimu ya sekondari iliyopewa
shilingi 614,474,000/= sawa na asilimia 16.
Tatu
Kisori pia amewasilisha bajeti ndogo ya maombi maalum ya nje ya ukomo
wa bajeti kutokana na baadhi ya shughuli muhimu kushindwa kuingia
katika bajeti kutokana na viwango vidogo vya bajeti vilivyowekwa na
TAMISEMI na hivyo kuathiri bajeti kushindwa kuingizwa vitu muhimu ili
kufikia malengo na kuondoa kero zilizoko katika jamii
Kisori
amesema kutokana na hali hiyo halmashauri imelazimika kuomba fedha nje
ya bajeti ya kawaida kiasi cha shilingi 3,558,000,000/= kwa ajili ya
kununulia gari la kuzoa taka ngumu mjini Mpanda, kununulia gari la
kunyonya maji machafu mjini, matengenezo ya gari la zimamoto na ujenzi
wa sekondari ya Kata ya Kakese pamoja na kuweka miundombinu ya umeme
katika shule za sekondari zote.
Aidha
baraza la madiwani la halmashauri ya mji Mpanda limeridhia na kupitisha
makisio ya bajeti ya hamashauri hiyo katika kipindi cha Julai 2012 hadi
juni 2013 kiasi cha shilingi 14,688,051,240/= ikiwa ni mapato ya ndani
na ruzuku ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ya Mji
Mpanda
Awali
akiwasilisha mapitio ya bajeti ya 2011/2012 Kisori amesema halmashauri
yake ilipanga kukusanya kiasi cha shilingi 823,164,000/= kutoka katika
vyanzo vya ndani na kuweza kukusanya kiasi cha shilingi 241,873,480/=
katika kipindi cha Julai 2012 hadi januari 2012 sawa na asilimia 29.38
ya makisio ambapo kiasi hicho kimefikiwa kwa kutumia mawakala wa
ukusanyaji wa ushuru.
Amesema
katika kipindi cha bajeti 2011/12 halmashauri ilipanga kuingiza mapato
ya shilingi 70,350,000/= kutokana na vyanzo vya mapato vilivyofutwa na
kuweza kukusanya shilingi 42,028,500/= sawa na asilimia 60 ya makisio.
Katika
hatua nyingine baraza hilo limetoa Baraka zote kwa shirika la nyumba la
Taifa kuenza ujenzi wa majengo katika mji wa Mpanda baada ya kuridhia
malipo ya shilingi milioni 100 ikiwa ni kwa ajili ya eneo la jingo la
starehe maarufu kwa jina la jengo la Paradise eneo litakalojengwa
gorofa nne kwa ajili ya matumizi ya kibenki, ofisi na maduka ya biashara
Aidha
baraza hilo limepokea na kuridhia maombi ya mamlaka ya viwanja vya
ndege nchini juu ya kuomba upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mpanda
utakaopelekea kuhamishwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo la Nsemulwa
Uwanja wa ndege ili kupisha upanuzi huo.
Imeelezwa
katika baraza hilo kuwa upanuzi huo taathiri baadhi ya wananchi
watakaotakiwa kipisha upanuzi huo baada ya kulipwa fidia na mamlaka
husika katika kipindi kifupi kijacho kwani ujenzi unatarajia kuanza
katika kipindi kifupi kijacho.Source Francis Godwin.
Comments