Mfanyakazi
wa kampuni ya Clouds Media, Said Bonge 'Bonge' akirekebisha singe
kwenye mnara wa askari katika makutano ya mtaa wa Samora na Azikiwe Dar
es Salaam jana. Singe hiyo ilikunjwa wiki iliyopita na mtu anayedaiwa
kuwa ni mgonjwa wa akili aliyetaka kuiangusha sanamu hiyo
inayolitambulisha jiji la Dar es Salaam.(Na Mpigapicha wetu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Comments