UNAPOWATAJA wachezaji sinema za mapigano au action huwezi kumwacha
msanii mwenye asili ya kiafrika, Billy Wayne Blanks ambaye ni raia wa
Marekani.
Blanks ni msanii mwenye umbo linaloonesha kuwa yuko fiti kimazoezi, alizaliwa Septemba 1,1955 katika eneo la Erie, Pennsylvania, Marekani, akiwa mtoto wa nne katika familia ya watoto 15.

Ni mtaalamu wa mazoezi ya viungo, sanaa ya mapigano, mwigizaji na mwanzilishi wa sanaa ya mapigano maarufu kama Tae Bo.
Alianza kujifunza sanaa hiyo akiwa mdogo na umri wa miaka 11 ambapo alijifunza sanaa ya mapigano ya Karate na Taekwondo.
Alizaliwa akiwa na ulemavu katika maungio kutoka kwenye mapaja kitu ambacho kimeathiri utembeaji wake na kufanya ndugu zake kumtania na kusababisha makosa na kuamini kuwa asingefanikiwa sana.
Mungu hatupi mja wake, waswahili walisema, Billy aliweza kukabiliana na changamoto hiyo ya kimaumbile na kuja kupata mafanikio katika karate. Alivutiwa na sanaa hiyo kutokana na kumwona kwenye televisheni msanii nguli aliyetamba kwa sanaa hiyo Bruce Lee, na mara moja akajiapiza kuwa lazima aje kuwa bingwa wa dunia wa sanaa hiyo.
Nidhamnu ya mazoezi ilianza kuutengenza mwili wake na kuwa fiti kwelikweli.
Aliingia katika uigizaji katika miaka ya 1980 ambapo aliigiza katika filamu kadhaa ambazo hazikufanya vizuri sana.
Kuna wakati alikodiwa kwua mlinzi wa mwingizaji mahiri Catherine Bach katika upigaji picha wa filamu ya Driving Force, hiyo ilitokana na halia ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa mjini Manila ufilipino wakati huo, akawavutia watararishaji filamu wakaamu kumwingiza katika muswada.
Mwishoni mwa miaka ya 1980, Blanks alianzisha sanaa ya mapigano aliyoopa jina la Tae Bo workout, ambapo aliendesha studio ya Karate Quincy, Massachusetts.
Katika sanaa yake hiyo Tae Bo, karate na ngumi hutumika, ni herufi za kwanzo za (tae kwon do na boxing).
Blanks alifungua kituo chake Los Angeles kuwafudisha watu waliokuwa wakitaka. Aliwavutia watu maarufu kama vile Paula Abdul na kisha sanaa yake kukua haraka na akaanza kutengeneza na kusambaza video na DVD ambzo ziliuzwa kwa wingi.
Alimwoa Gayle H. Godfrey, ambaye alikutana naye katika madarasa ya karate. Binti wa Gayle, Shellie, alizaliwa Juni 28, 1974, aliasiliwa muda mfupi baada ya kuolewa.
Baadhi ya kazi zake alizocheza ni Jack & Jill (2011)
Sabrina, Tamthilia ya televisheni the Teenage Witch, Guest star (Prelude to a Kiss) (1999),Virtual Kickboxing (1998), Tamthilia ya TV BattleDome (1998)
Kiss the Girls (1997), Balance of Power (1996)
Expect no Mercy (1995), Back in Action (1994),
Tough and Deadly (1994) na Showdown (1993).
Kazi nyingine alinzoanza nazo ni TC 2000 (1993),
Talons of the Eagle (1992), Zhan long zai ye (1992)
The Last Boy Scout (1991), Timebomb (1991),
The King of the Kickboxers (1991), Bloodfist (1989) na Low Blow (1986)
Shellie Blanks Cimarosti naye kwa sasa ni mtaalamu wa sanaa ya mapigano na yumo kwenye mikanda ya video mafunzo ya Billy ya Tae Bo na pia akaribuni alitengenza video yake ya Tae Bo Postnatal Power.
Gayle na Billy pia wana mtoto wao wa damu, Billy Blanks Jr. ambaye ni dansa, mwimbaji na mtaalamu wa mazoezi ya viungo akiwa ametengeneza DVD nyingi zilizouzwa sana ikiwemo ya "Cardioke" & "Fat Burning Hip Hop Mix", amewahi kufanya kazi na wanamuziki Madonna, Quincy Jones na Paula Abdul akiwa kama dansa katika video zao.
Billy na Gayle walitalikiana mwaka 2008 baada ya kwua katika ndoa kwa miaka 33.
Gayle alifungua kesi ya kuomba talaka katika Mahakama Kuu Los Angeles Aprili 22, 2008, alikuja kutengana rasmi na Septemba 25, 2007 ambapo sababu kuu ya kutengana ikitajwa kuwa ni 'fofauti zisizorekebishika."

Comments