Ndugu zangu,
Nchi
yetu inaingia gharama zisizo za lazima kama ambazo nchi inaingia kwa
sasa kwa wagombea, vyama na hata Serikali kutumia fedha nyingi katika
chaguzi ndogo. Tumeona hata helikopta zenye gharama nyingi zikiruka
kilomita nyingi angani eti kwenye harakati za kusaka kura kwenye
chaguzi ndogo huku wananchi wengi wa jimbo husika wakitembea kilomita
nyingi kusaka maji ya kunywa na kupikia.
Wiki
kama hii ya Maji inayoendelea sasa ilipaswa kuwa wiki ya kuomboleza
uhaba wa maji unaochangiwa pia na matumizi mabaya ya rasilimali za
wananchi kama haya ya kuendesha chaguzi ndogo kule Arumeru Mashariki. Na
hili ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.Inatoka kwa mdau Mjengwa.
Comments