Skip to main content

Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar Balozi Seif Iddi:CCM Itaheshimika Endapo Viongozi Watatekeleza Wajibu Wao


Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akikifungua Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Hapo Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.Kulia yake ni Katibu wa UVCCM Mkoa Mjini Magharibi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mh. Tauhida Galos Nyimbo
Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Mjini Magharibi
--
Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuheshimika ndani ya Jamii endapo Viongozi wanaokisimamia kuanzia ngazi ya Shina hadi Taifa watatekeleza vyema wajibu wao kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Mjini Magharibi uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Balozi Seif alisema huu si wakati wa kutomuonea haya Mtu ye yote anayeendeleza tabia za kudhoofisha Chama ambae hujihisi kwamba madaraka aliyopewa na Wanachama ni yake Binafsi.

Aliwaomba Vijana hao wa CCM kuwakaba Viongozi wasiotaka kutekeleza majukumu yao ndani ya Matawi na Majimbo yao kwa lengo la kukisafisha Chama hicho ili kiendelee kuwa kimbilio la Wanyonge.

“ Chaguzi hizi zinazoanza ndani ya Chama ni vyema zikawa chanzo cha kusafisha Chama kwa kuwaacha watu wenye sura mbili katika Uongozi”. Alitanabahisha Balozi Seif.

Akizungumzia Utekelezaji wa Ilani ya Chama ya Mwaka 2010 ndani ya Serikali Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali itahakikisha kwamba wale wanaokwenda kinyume na azma ya Serikali pamoja na Ilani hiyo wanachukuliwa hatua.
Alisema lengo la Serikali ni kuwapatia huduma bora wananchi kwa Mujibu wa Sheria na Taratibu zilizowekwa.

“ Tumekubali kuwa na Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa nia ya kutandika Demokrasia makini ndani ya Jamii kupitia Ilani iliyoridhiwa na Wapiga kura . Hivyo Mtendaji asiyekubali 

mfumo huo ni vyema akajiondoa mwenyewe Madarakani” Alionya Balozi Seif.
Mapema Katika Taarifa yao iliyosomwa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Ndugu Mgeni Mussa Vijana hao walisema Serikali inapaswa kuwatenga Watendaji wasiotaka kufuata Ilani ya Chama ya mwaka 2010 katika utekelezaji wa Majukumu waliyopangiwa na Taifa.

Vijana hao pia wameipongea Serikali Kuu kupitia Kamati ya Maafa Zanzibar kwa umakini wake katika harakati za uokozi kwenye janga la Kuzama kwa Meli ya M.V Spice Islanders mwezi Septemba mwaka 2011.

Kikao hicho cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Mjini Magharibi kiliambatana pia na Semina iliyojumuisha mada mbili ambazo ni Uwezo wa Vijana ndani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Mchakato wa kuelekea kwenye Katiba Mpya ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Seif akiwa pia Mbunge wa Jimbo la Kitope amekabidhi Mabati Mia moja na Ishirini pamoja na vifaa vyake vyote vya kuezekea kwa ajili ya Tawi la Chama Cha Mapinduzi la Kitope A vikiwa na gharama ya Shilingi milioni tano.

Akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kitope A Ndugu Mikidadi Adam Mbunge huyo wa Kitope amewapongeza Wanachama wa Tawi hilo kwa uwamuzi wao wa Kujenga Tawi lenye hadhi ya Chama chao.

Baadaye Balozi Seif akakabidhi Mabati Mia Mbili na Thalathini na Mbili yenye thamani ya Shilingi Milioni Nne kwa ajili ya kusaidia nguvu za Wizara ya Elimu Kuliezeka Jengo Jipya la itakayokuwa Skuli ya Msingi ya Matetema iliyopo Kazole.

Mabati hayo amemkabidhi Sheha wa Shehia ya Matetema Bwana Mohd Bakar Mohd na kusema kitendo cha Wananchi hao cha kuwapunguzia masafa marefu watoto wao kutafuta Elimu kinafaa kuigwa na Maeneo mengine.

Jengo hilo la Skluli ya Matetema lenye madarasa manne, Ofisi ya mwalimu Mkuu na Stoo linatarajiwa kuezekwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar muda si mrefu.


Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 10/3/2012.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...