Ni kupitia kampeni ya Red Alert na Vodacom M-pesa.
Dar es salaam 12 Disemba 2012. Kampeni iliyoendeshwa na kampuni
ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kuchangisha
fedha kupitia Red Alert na M-pesa imewezesha kupatikana kwa shilingi
11,607,470/=
Kampeni hiyo iliyodumu kwa wiki tatu kuanzia Disemba 22 mwaka jana hadi
Januari 10, 2011 imewezesha kupatikana fedha hizo zilizochanganywa na
wateja kuunga mkono juhudi za Vodacom za kusaidia waathirika wa maafa.
Kampuni ya Vodacom ilitangaza kuwashwa kwa nambari ya Red Alert na
kuweka nambari maalum ya kuchangia kwa M-pesa saa chache baada ya
kutolewa taarifa rasmi za kuwepo kwa athari kubwa za mvua zilizonyesha
kwa siku tatu mfululizo Dar es salaam.
“Kila mtu alikuwa na nafasi ya kusaidia kuokoa na kusitiri maisha ya
wenzetu waliothiriwa na ndio maana tukawasha nambari ya Red Alert na
kuruhusu uchangiaji kupitia M-pesa” Amesema Ofisa Mkuu wa Masoko na
Mahusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Mwamvita Makamba.
Nambari ya Red Alert hutumika na Vodacom wakati wa maafa kuwezesha
wateja kuchangia fedha kusaidia waathirika na hakuna makato
yanayofanywa katika ujumbe mfupi unaotumwa katika nambari hii ili
kiwango kinachopatikana kiwanufaishe waathirika moja kwa moja.
Maafa yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha sehemu mbalimbali nchini
ikiwemo Dar es salaam Disemba mwaka jana yaligharimu maisha ya watu
huku maelfu ya familia yakiachwa bila makazi.
“Ni jambo la faraja kwamba tumeweza kusimama kama familia moja ya
Vodacom wafanyakazi, wateja wetu na wadau na kuonesha upendo wetu
dhidi ya wenzetu walioguswa na maafa hayo”. Aliongeza Mwamvita.
Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusiadia jamii –
Vodacom Foundation inaandaa utaratibu wa michango hiyo kuwanufaisha
walengwa kama ilivyokusudiwa.
Awali Vodacom Tanzania ilichangia vitu mbalimbali vyenye thamani ya
shilingi milioni thelathini ikiwemo vyakula, magodoro na mablanketi kwa
waathirika wa maafa ya Dar es salaam waliokuwa wakiishi katika kambi
maalum kwa wakati huo.
Ujumbe mmoja wa maneno kwenda nambari ya Red Alert 15599 uligharimu
Tzs 500/-, na kwenda M-pesa nambari 155990 uligharamiu Tzs. 1,000/- na
kwamba hakukuwepo na ukomo wa kutuma ujumbe na kuchangia.Inatoka kwa Mdau Mjengwa.
Comments