Serikali yapewa saa 72 kuwarejesha madaktari Muhimbili Dk. Mtasiwa asimamishwa uanachama kwa mwaka mmoja JK atakiwa kuwatafutia kazi nyingine Nyoni, Dk. Mtasiwa.
Na Richard Mwaikenda
CHAMA
cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeipa Serikali saa 72, kuwarejesha
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Wanafunzi waliofuzu udaktari waliondolewa
hapo baada ya kugoma wakidai malipo yao.
Tamko hilo lilitolewa na Rais wa chama hicho, Dk Namala Mkopi katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana.
Chama
hicho kimemuomba Rais Jakaya Kikwete, kuwatafutia kazi nyingine, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga
Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa kwa kosa la kumshauri vibaya Waziri
wa wizara hiyo, Dk. Hadji Mponda. Alisema Dk. Mponda anasamehewa kwani
hajui alitendalo ila inatakiwa awaombe radhi kwa kuwaita madaktari
wenzao kuwa si madaktari bali bado wangali wanafunzi.
Rais wa
MAT, Dk. Mkopi, pia alitangaza kuwa kimefutia uanachama kwa mwaka
mmoja, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mtasiwa kwa kosa lake la kuusaliti
udaktari kutokana na kukiuka kiapo cha udakatari kinachosema kuwa
Madaktari wote ni ndugu na nitawatendea haki kama dada na kaka.
Alisema
endapo Dk. Mtasiwa atanendelea na tabia hiyo ya kudharau taaluma ya
udakatari, basi chama kitaamua kumfukuza kabisa na kumuweka kwenye
mtandao wa madaktari duniani, ili iwe fundisho kwa madaktari wengine
wenye tabia hiyo.
Dk. Mkopi alisema kuwa chama kimesikitishwa
sana na kwamba hawaoni ni kwa nini Serikali imeamua kuwaadhibu
madaktari wenzao waliokuwa wakidai haki ya msingi, na kuwaacha
kuwaadhibu watu waliosababisha ucheleweshaji wa makusudi wa kutowalipa
malipo yao madaktari.
Aliwataka viongozi kuacha tabia ya kutumia
siasa kuingilia masuala ya kitaaluma, na kwamba wanavyofanya hivyo,
wajue kwamba wanaowakomoa si madaktari bali ni wagonjwa. Alisema
kitendo cha kuwaondoa madakari zaidi ya 200 tayari kimeanza kuleta
athari kwa madakatari mabingwa waliokuwa wakisaidia kazi, na kwamba
kibaya zaidi kusababisha wagonjwa wengi kufariki katika Hospitali hiyo.
Alisema
kitendo cha Serikali kuwaondoa madaktari wenzao katika Hospitali ya
Muhimbili na kuamua kuwapangia Hospitali zingine si kizuri, kwani
baadhi ya hospitali walizohamishiwa hakuna nafasi wala mambo
wanayotakiwa kujifunza, hivyo mpaka sasa hakuna wanalolifanya.
Chama
hicho, kimeitisha mkutano mkubwa wa madakari wote nchini, Jumatano
ijayo utakaofanyika, Dar es Salaam, na kuzungumzia mambo kadhaa
likiwemo la madakatari wenzao.
Alitaja baadhi ya ajenda
watakazozungumzia kwenye mkutano huo, kuwa ni;Hatima ya heshima ya
udaktari, Ulipaji posho kwa madaktari, Mshahara uendane na elimu,
majukumu na hadhi ya udaktari, madaktari kupewa nyumba, posho ya
mazingira magumu, posho ya mazingira hatarishi pamoja na uhamishaji
ovyo wa madaktari. |
Comments