Msimu
wa wasanii Tanzania Kuvuna Walichokipanda kati ya mwaka 2011 maana
Tunzo pekee Nchini Zijulikanazo kama Basata Kilimanjaro Music Awards
zimewadia na tayari mchakato huo umezinduliwa rasmi ..Kwa mujibu wa
ratiba iliyotangazwa, wanamuziki waliofanya vizuri mwaka jana kwa ajili
ya kupewa tuzo mwaka huu, watachambuliwa kwenye Academy ya siku mbili
kama ambavyo hufanyika kila mwaka.Taarifa kwa vyombo vya habari,
iliyosomwa na meneja wa kampuni wadhamini wa Kili Music Awards, George
Kavishe imeeleza kwamba kwenye academy ndipo wanamuziki watapagwa
kwenye vipengele (categories) tofautitofauti.Kavishe alisema, academy
itafanyika kati ya Januari 26 na 27 ambapo wadau kati ya 50 na 100,
watakutana na kuchanganua wanamuziki wa aina zote, waliofanya vizuri
mwaka jana na kuwekwa kwenye vipengele vyao kabla ya kuruhusu
Watanzania wapige kura kuwapata wale watakaotunukiwa tuzo hizo.Alisema,
kura za Watanzania zitabeba uzito wa asilimia 70 na majaji 15 watakaa
kama jopo na kusimamia watu watakaoshinda ili wawe ni wale kweli
wanaostahili.Alifafanua kwamba uzito wa kura za majaji 15, ni asilimia
30....
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu

Comments