Na: Kitengo cha Habari
WHVUM
Dar es Salaam
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema
kuwa Tanzania inafurahia uhusiano uliopo kati yake na China hususan
katika tasnia ya Utamaduni.
Waziri
Nchimbi ameyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati akiongea na
kikundi cha sanaa cha Tianjin kilichotoka nchini China kushirikiana na
jamii ya kichina inayoishi nchini kusherehekea mwaka mpya wa Kichina
ujulikanao kama ‘Spring Festival.’
Aidha,
Kikundi hicho kilichoambatana na Balozi wa China, Bw. Liu Xsheng
kimeishukuru Serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa ushirikiano ambao
imekuwa ikitoa katika masuala mbalimbali ya Utamaduni na maendeleo ya
nchi hizo mbili.
“Tunaishukuru
Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikitoa katika
masuala mbalimbali ya utamaduni na maendeleo baina ya nchi hizi
mbili”.Alisema Balozi Liu Xsheng ambae aliongozana na kikundi hicho.
Ugeni
huo umetumia nafasi hiyo kumkaribisha Dkt. Nchimbi kushiriki Tamasha la
Utamaduni la Afrika (African cultural forum) litakalofanyika nchini
China Mei mwaka huu.
Kikundi
hicho kilimtembelea leo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
kwa ajili ya kutoa shukurani kwa Wizara kwa ushirikiano iliyoonyesha
wakati wa maandalizi ya sherehe hizo.
Comments