KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BASATA WAZINDUA RASMI MCHAKATO WA TUNZO ZA MUZIKI TANZANIA 2012(KILI MUSIC AWARDS).
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro Premium Lager kwa
kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo
wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa
Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa
2012.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam meneja wa bia ya
Kilimanjaro bwana George Kavishe alisema Mwaka jana Tunzo hizi za
Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo kwa mwaka
huu yataendelezwa na kuboreshwa zaidi. Ambapo Mchakato wa kuwapata
vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:
1. ACADEMY:
ACADEMY
ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya
hamsini hadi mia moja( 50 mpaka 100)kutoka mikoa mbali mbali ya
Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua
na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya
majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekizi vigezo
vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika
tarehe 27 na 28 Jan 2012.
2. Majaji:
Hatua
ya pili ni Majaji ambapo huwa ni hatua muhimu sana ambapo majaji huwa
na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya
kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa
katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura
zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali
vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka
2011, kazi zao za mwaka 2011, Mafanikio n.k. Jopo hili hujumuisha wadau
wa tasnia ya musiki kumi na tano (15).
3. KURA:
Hii
ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa musiki waliopiga kura zao Kura
hizo hujumuishwa katika kuchangua washindi ambapo kwa shindano la mwaka
huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia sabini
(70%) na kura za majaji asilimia thelasini (30%.) na katika kufanikisha
upigaji kura kutakuwa njia kuu Njia kuu nne za upigaji wa kura :
- Njia ya ujumbe mfupi (sms).
- Njia ya barua pepe (Email).
- Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
- Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)
Kwa
upande wake mwakilishi wa baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mzee Luhaja
amewataka wasanii wa tasnia hiyo nchini kutumia vyema fursa ya tunzo za
Kili Music Award kama sehemu ya kuweza kujitangaza katika anga za
muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
Alisema
msanii mzuri ni Yule anaeweza kutunga nyimbo zenye lengo la kuelimisha
jamii na kuburudisha kwa kuzingatia maadili na hayo hujidhihirisha
kupitia kwenye tunzo kama hizi ambazo hutoa fursa kwa wasikilizaji
kutoa michango yao juu ya mwanamuziki gani aliyeweza kukonga mioyo yao
kupitia tungo zake.Inatoka Full Shangwe.
Comments