Hii
ni sehemu ya tano ya simulizi. Pichani ni kijijini Isimani. Nje ya
nyumba ya marehemu Said Mwamwindi. Pamejengwa kumbukumbu ya kifo cha
Dr. Kleruu.
UKIMWONA
kwenye mitaa ya Iringa bado anatembea kwa hatua za kijeshi. Ni Mzee
David Butinini. Alipata kuwa askari polisi na alishuhudia kwa macho
yake, siku Mkulima Said Mwamwindi alipofika kituo cha Polisi Iringa
akiwa na mwili wa marehemu Dk. Kleruu kwenye gari aliloendesha.
Dk.
Kleruu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeuawa na Mwamwindi kwa
kupigwa risasi. Mzee David Butinini alikuwa pia mmoja wa mashahidi
kwenye kesi ya mauaji iliyomkabili marehemu Mwamwindi.
Mzee
David Butinini ni rafiki yangu wa muda mrefu. Jioni ya Jumapili moja
tunakutana Soko Kuu Iringa. Namuuliza juu ya kumbukumbu zake ya
kilichotokea miaka 40 iliyopita.
Tunazungumza
huku kwa pamoja tukikiangalia kituo cha polisi kilicho mbele yetu na
ambapo Mzee David Butinini alifanya kazi kama Polisi miaka 40
iliyopita.
“Unasikia
Maggid, nilishuhudia kwa macho yangu. Nilikuwa bado kijana enzi hizo.
Nilikuwa mwanamichezo pia. Nilikuwa kwenye kikosi cha polisi cha mpira
wa miguu. Nakumbuka ilikuwa jioni ya Jumapili ya Krismasi . Ni kwenye
saa kumi na moja hivi.
Tulikuwa kama askari watatu hivi tumevalia kiraia na tulisimama pale
nje ya kituo,” Mzee David ananieleza huku akionionyesha kwa mkono
mahali hapo.
Kelele
za makuli wabeba mizigo sokoni zinatufanya mimi na Mzee Butinini
tusisikilazane vema. Wote, kutokana na utamu wa simulizi hii tunajikuta
tunasogea mbele kidogo na kusimama kando ya kibanda cha rafiki yangu
Mwarami. Kijana anayeuza matunda Soko Kuu la Iringa.
“Unajua Maggid,.... Soma zaidi; http://www.raiamwema.co.tz/kwa-nini-mkulima-mwamwindi-alimpiga-risasi-rc-dk-kleruu-v
Comments