Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema,
aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto
Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani
kwao Ifakara kwa maziko. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho
kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu
Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la
Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17,
katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa
kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali. Picha na Muhidini Sufiani wa OM
Spika
wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake
za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.
Kutoka
kulia ni Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta, Mama Tunu Pinda mke
wa Waziri Mkuu, Mwantumu Mahiza Mkuu wa mkoa wa Pwani na Naibu Spika wa
Bunge Job Ndugai. Picha Owen David
Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.
Waombolezajio wakishuhudia mwili wa marehemu Regia Mtema wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee tayari kwa kuagwa leo.
Source:Full Shangwe

Comments