NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
IMEELEZWA
kuwa pamoja na nchi kukabiliwa na majanga na changamoto mbalimbali hasa
kwa mwaka 2011 wakristo hawapaswi kukata tamaa juu ya changamoto hizo
bali wanatakiwa kuangalia imani na mahitaji ya Mungu Kwa mwanadamu ili
aweze kupunguza na kuondoa changamoto hizo.
Hayo yameelezwa mjini hapa na mchungaji Simion Vomo wakati akiongea na waumini wa kanisa la T.A.G Christian All Nation Church lilopo katika manispaa ya mji wa arusha mapema wiki hii.
Aidha
mchungaji Vomo alisema kuwa katika mwaka 2011 mambo mengi sana
yalijitokeza hali ambayo iliwapelekea baadhi ya waumini kukata tamaa
lakini katika mwaka huu mpya wa 2012 wanapaswa kumuangalia mungu zaidi
kuliko matatizo yao binasi.
Alibainisha
kuwa hata katika matatizo mungu yupo na kwa hali hiyo kila mwanadamu
anapaswa kuangalia mpango na mikakati mbalimbali ya mungu na kuachana
na tabia ya kuona wameshindwa mbele ya Macho ya wanadamu
Awali
alisema kuwa nao waliofanikiwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatangaza
zaidi utukufu wa mungu kuliko mafanikio yao kwa kuwa ndicho chanzo
pekee cha kufanikiwa katika maitaji mbalimbali ambayo yanamzunguka
mwanadamu wa leo.
Alibainisha
kuwa endapo kama wataweza kufanya hivyo ni wazi kuwa mafanikio yatakuwa
ni makubwa sana ukilinganisha na mafanikio ambayo hayana utukufu wowote
hapa duniani.
Alimalizia
kwa kusema kuwa kwa wale ambao hawajafanikiwa kwa msimu wa mwaka
uliopita wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaongeza kiwango cha imani
katika maisha yao kwa kuwa Pia Mungu anapenda na kuthamini zaidi Mtu
mwenye Imani.Inatoka fullshangwe.
Comments