Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa
Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini
(CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam jana jioni Januari 15
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwa
Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na
City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko
yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana,
ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa
Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana
Januari 15.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa
Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na
Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya
kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya
sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15. Picha na Muhidin
Sufiani-OMR kwa hisani ya mdau Mjengwa.
Comments