Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika
Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu
Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika leo kwenye kanisa hilo na
kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi
ya wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda
kanisani hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla ambapo
FULLSHANGWE ilishuhudia tukio hilo.
Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki
na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa
amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu
alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka
jana hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu
kwa miujiza yake.
Waziri
wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo na
kumkaribisha Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumza machache na waumini
wa kanisa hilo na kutoa ushuhuda wake.
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo leo.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada leo.
Comments