Wabunge
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge
wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya
kuwasilisha mchango wao kwa timu hiyo.
Benchi
la Ufundi la Twiga Stars kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limekubali kucheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya maonesho tu
ambapo baada ya kumalizika ndipo Wabunge watakabidhi kile walichopanga
kutoa kwa timu.
Mechi
hiyo itafanyika Alhamisi (Januari 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume uliopo Ofisi za TFF kuanzia saa 10 kamili jioni.
Comments