Mkuu wa Mkoa wa DSM Said Mecky Sadick (kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni tano
(5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto)
leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es
Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO),
MISAADA BADO INAHITAJIKA
(5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Fadhili Manongi (kushoto)
leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa DSM kwaajili ya waathirika wa mafuriko wa mkoa wa Da r es
Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO),
MISAADA BADO INAHITAJIKA
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
16/1/2012
MKUU wa mkoa wa Dares Salaam Said Mecky Sadick amesema bado misaada zaidi inahitajika ili kuweza kuwasaidia wahanga wa mafuriko hususan ya shughuli za ujenzi na mahitaji ya watoto walioanza shule.
Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Sadick wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jijini Dares Salaam mara baada ya kupokea msaada wa hundi ya sh. milioni tano kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, ambayo ilikadhiwa kwake na Mkurugenzi Mkuu Fadhili Manongi.
“Bado
misaada inahitajika tunaendelea kutoa wito kwa watu walioguswa kuweza
kutoa michango yao ili kuweza kusaidia shughuli za ujenzi na mahitaji
ya wanafunzi walianza shule mfano madaftari, vitabu na huduma zingine
zinazohusiana na elimu,” alisema.
Aliongeza kuwa changamoto nyingine iliyopo
ni kujenga nyumba za walimu na kliniki ya wakinamama na watoto,hivyo
aliwaomba Watanzania, taasisi, mashirika na watu binafsi walioguswa kuendelea kuchangia.
Wakati huohuo, Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (CBCT),kilikabidhi hundi kivuli yenye thamani sh. milioni 10 ya michango ya vitu mbalimbali kwa ajili ya wahanga hao kwa Mkuu huyo, ambayo ilikabidhiwa katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina kwa Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal juzi usiku.
Hundi hiyo ilikabidhiwa
kwa Sadick na Mwenyekiti wa CBRT Zhu Jinfeng, ambapo alisema misaada
mingine imendelea kutolewa hivyo michango hiyo hadi leo(jana) imefikia
sh. milioni 12,550,000.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa alisema agizo la kuangalia uwezekano wa kuwapatia
viwanja wapangaji liko palepale na watalitekeleza kama alivyoagiza Rais
Jakaya Kikwete, hivyo utaratibu utaanza mara baada kukamilisha zoezi la
wamiliki.
Aliongeza kuwa utaratibu huo wa wapangaji pia unahitaji fedha kwa ajili ya kufanya tathimni mpya utoaji wa fidia kwa wananchi watakaopisha maeneo hayo.
Comments