JOHN TENDWA
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MSAJILI wa Vyama Vya Siasa, John Tendwa amesema kwamba ofisi yake inafikiria kuweza kubadilisha mifumo ya uchaguzi kwa kufikiria nafasi na haki za msingi za mpigakura dhidi ya chama kinapomfukuza uanachama mbunge.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Tendwa wakati akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dares Salaam mara baada ya kuapishwa kwa
viongozi wapya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ambapo alisema suala
la kufukunzwa uanachama mbunge si geni lilishatokea hata katika mfumo
wa chama kimoja.
Tendwa alitoa kauli hiyo mara baada ya kuulizwa swali la waandishi wa habari kuhusiana na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid kufukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) hali ilimfanya kupoteza nyadhifa zake.
Ambapo Tendwa aliongeza kuwa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi inapotokea hali ya namna hiyo , alihoji kuwa mpigakura anafikiriwaje na chama juu ya sifa na haki za msingi dhidi ya chama.
“Tunafikiria tuweze kubadilisha mifumo hiyo ya uchaguzi kwa kuangalia mbunge na lazima tumfikirie mpigakura. Lazima tuangalie hali ya uchumi,” alisema Tendwa.
Alisema kitendo hicho kinasababisha gharama kwa serikali na wadau wengine mfano taasisi yake ambayo haikutarajiwa hata katika bajeti.
Tendwa
aliongeza kuwa inapotakiwa kufanyika uchaguzi mwingine zinahitajika
fedha nyingi ambapo wakati fulani alisema zinaweza kufikia sh. bilioni 19 ,hata hivyo hazitoshi.
Aidha alisema kuwa kifedha bado kitendo hicho kililiweka taifa katika mshtuko mkubwa kwa kuwa gharama ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine ni kubwa.
Alihoji kuwa maamuzi hayo yanapofanyika hawakuona fursa ya mpigakura ana haki gani ya kumtambua mbunge wake? je chama kinafaidika nini?
Alisema wataangalia kama taratibu zilifuatwa na chama ili waweze kushauri
Tendwa
alisema suala hilo limekuwa ni tabia na desturi, hivyo ni jambo
linapaswa kuangalia mbele ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa kwa kuwa
kitendo hicho si kujenga demokrasia bali ni kuwafanya wanachama kuwa na
utii wa uwoga ndani ya chama.
Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki
,John Cheyo akizungumzuia suala hilo alisema kitendo hicho cha
kumwondoa mbunge katikati ya muda kinaleta matatizo makubwa ndani ya
vyama , hivyo alivishauri vyama kuheshimu sheria na taratibu za mtu kumaliza muda wake.
Hivi karibuni Chama cha NCCR – MAGEUZI nacho kilimvua uanachama, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila kwa madai ya utomvu wa nidhamu.

Comments