DKT BILAL AZINDUA JENGO LA UTAWALA LA SHULE YA SEKONDARI MNOLELA, AKAGUA UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA KINENG’ENE-LINDI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati alipowasili kwenye shule ya Sekondari ya Mnolela, alipofika kuzindua Jengo la Utawala la shule hiyo, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi, Januari 21, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo jipya la Utawala la Shule ya Sekondari Mnolela, iliyopo kijiji cha Luhokwe, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi juzi Januari 21, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Uwanja wa Fisi Lindi juzi Januari 21, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe, Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili baada ya Makamu
kumaliza kuwahutubia wananchi wa Uwanja wa Fisi, mkoani Lindi juzi
Januari 21. Picha na Muhidin Sufiani-OMR .Inatoka wa mdau Mjengwa.
Comments