Baadhi
wa wakandarasi kutoka kampuni ya ya Strabag International Gmbh ya
Ujerumani wakisubiri kuweka saini mkataba wa ukarabati wa barabara ya
kutoka Korogwe- Mkumbara- Same katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya
ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) jijini Dar es Salaam
Jan,26.2012. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akitoa taarifa ya
mradi wa ukarabati wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same (km 172)
jijini Dar es salaam katika hafla ya uwekaji saini Jan,26,2012, (Picha
na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akiwekeana saini
mkataba wa ukarabatiwa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same pamoja na
Mkandarasi kutoka kampuni ya Strabag International GmbH ya Ujerumani
Meneja Biashara kwa Afrika Mashariki Bw Karl Henz Schneder, (kulia) leo
jijini Dar es Salaam, Hafla hiyo pia imeshudiwa na Waziri wa Ujenzi
Dkt, John Magufuli (katikati alievaa miwani) akifuatiwa na Makamu
Mwenyekiti Kamati ya Miundombinu ambae pia na Mbunge wa Same Mashariki
Anne Kilango Malecela, pamoja na watendaji wa ngazi za juu wa Wizara ya
Ujenzi na wadau wa sekta hiyo,Ukarabati huo wa km 172 utagharimu zaidi
ya shilingi bilioni 128 za kitanzania, ambapo kampuni hii itakarabati
kipande kutoka Korogwe- Mkumbara (76 km) na kugharimu zipatazo shilingi
bilioni 63 Hafla hiyo imefanyika Jan, 26,2012( Picha na Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale
(kushoto) pamoja na Mkandarasi kutoka ya DOTT Services Ltd kutoka
Uganda ambae ni Meneja Mkuu Bw.G,Prudhvi Raj wakiwekeana saini mkataba
wa ukarabati wa ujenzi wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same leo
jijini Dar es Salaam, Mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi 12
bilioni. ambapo kampuni hii itakarabati kapande cha Mkumbara- Same (96
km) kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 65 za kitanzania,(Picha na
Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akibadilishana hati
na Mkandarasi , kutoka kampuni ya Strabag International GmbH ya
Ujerumani ambae ni Meneja Biashara kwa Afika Mashariki Bw, Karl Henz
Schneder leo jijini Dar es salaam baada ya kusaini mkataba wa ukarabati
wa barabara ya Korogwe- Mkumbara- Same ya km 172 ambayo itagharimu
zaidi ya shilingi bilioni 12 za kitanzania. Lakini kampuni ya Strabag
itakarabati eneo la Korogwe- Mkumbara (km76) na itagharimi shilingi
62,866,110,284. Hafla hii imefanyika leo,Jan 26. 2012,(Picha na
Mwanakombo Jumaa-Maelezo).
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) wakibadilishana
hati ya mkataba baada ya kusaini na Mkandarasi kutok a kampuni ya DOTT
Services Ltd kutoka Uganda ambae ni Meneja Mkuu kwajili ya kukarabati
Mkumbara- Same (96km) utakaogharimu shilingi 65,129,670,563,82 za
kitanzania, leo jijini Dar es Salaam-Picha na Mwanakombo Jumaa-MALEZO.
Comments