Anthony Kayanda, Kigoma
POLISI
mkoani Kigoma wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mamia
ya wafuasi wa chama cha NCCR Mageuzi waliokuwa kwenye mkutano ambao
ulipaswa kuhutubiwa na mbunge Kigoma Kusini, David Kafulila.
Habari
zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi
katika Kijiji cha Kazuramimba ambako Kafulila alikuwa amejiandaa
kufanya mkutano wa hadhara na tayari alikuwa ameanza kuhutubia akiwa
kwenye gari na madiwani wawili wa chama hicho cha upinzani.
Kafulila
aliliambia gazeti hili jana kuwa polisi hao walizuia mkutano wake na
kumkamata kwa mahojiano yaliyodumu kwa takriban dakika 30, kwa madai
kwamba mkutano wake haukufuata taratibu za kuomba na kupata kibali.
Kafulila
ambaye yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kichama, alisema alipofika
kijijini hapo alipata taarifa kwamba polisi wa kituo kidogo kilichopo
eneo hilo waliwazuia viongozi wa NCCR Mageuzi kufanya maandalizi ya
mkutano huo.
Alisema
baada ya kusikia uamuzi huo, alilazimisha wafanye mkutano kwa vile yeye
ni mbunge halali wa jimbo hilo la Kigoma Kusini na anapaswa kuzungumza
na wananchi kuelezea utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja
uliopita.
“Polisi
wamenizuia kufanya mkutano wangu na wametumia nguvu kubwa kututawanya
kwa madai kwamba wametumwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kigoma (OCD),
Japhet Kibona eti sisi hatujatimiza masharti..., na pia hatujaomba
kibali cha kufanya mkutano. Sasa mimi kama mbunge wa jimbo nazuiliwa
kwa nini?," alihoji Kafulila na kuendelea:
"Inawezekana
huyu OCD ananihujumu na tayari nimewaeleza wakuu wake wa kazi kuanzia
IGP, Said Mwema na Waziri wa Mambo ya ndani, Shamsi Vuai Nahodha ili
wajue hujuma ninayofanyiwa na huyu OCD wa Kigoma,"alisisitiza
Kafulila..soma zaidi www.mwananchi.co.tz
Comments